1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tiger bado ni mahiri

15 Aprili 2019

Baada ya ukame wa miaka kumi na moja bila taji lolote kuu, hatimaye gwiji wa mchezo wa gofu Tiger Woods kutoka Marekani hapo Jumapili aliweza kulishinda taji la Masters.

https://p.dw.com/p/3GnmR
Golfsport Tiger Woods Sieger beim Masters in Augusta
Picha: picture-alliance/abaca/Atlanta Journal-Constitution/TNS/C. Compton

Hii ni mara ya tano Tiger kuvikwa koti la kijani ambalo ni ishara ya mchezaji ambaye ni bingwa wa shindano hilo.

Tiger amepitia kipindi kigumu kabla kuebuka mshindi tena kwani miaka michache iliyopita alikuwa amekata tamaa ya kuucheza tena mchezo huo baada ya kufanyiwa upasuaji na pia kuathirika na mambo ya kinyumbani.

Golfprofi Tiger Woods beim Masters in Augusta
Picha: Getty Images/A. Redington

"Mashindano haya yamekuwa muhimu sana kwangu kwa miaka mingi iliyopita. Nilikuwa na mashaka makubwa baada ya yaliyotokea miaka kadhaa iliyopita, nilikuwa siwezi kutembea, siwezi kuketi, sikuweza kulala, yani sikuweza kufanya chochote," alisema Tiger. "Yote yaliyofanyika leo, kulikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa na nafasi ya kushinda lakini kurudi hapa na kucheza vyema na kufanya vyema kila kitu ni jambo ambalo siwezi kulisahau," aliongeza gwiji huyo.