1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tishio la Usalama Marekani

30 Oktoba 2010

Vifurushi vilivyokuwa vikielekea Marekani vyagunduliwa kuwa na miripuko.

https://p.dw.com/p/PuLu
Rais Barack Obama wa Marekani.Picha: AP

Marekani imedhibitisha kuwa  miripuko  iligunduliwa   katika vifurushi viwili , vilivyokuwa vinaelekea   nchini  humo. Rais Barack Obama amesema  katika mkutano  na  waandishi habari  uliofanyika katika ikulu  kwamba vifurushi hivyo vilikuwa vinatarajiwa kupelekwa  katika  maeneo mawili ya kuabudu ya Wayahudi mjini Chicago. Pia amesema kuwa vifurushi hivyo vilitoka Yemen na viligunduliwa Dubai na Uingereza.

Wizara ya usalama wa ndani  nchini  Marekani ,imesema inaimarisha hatua za kiusalama kutokana na tishio hilo.

Kwengineko ndege za kivita za Marekani zimeisindikiza ndege ya abiria ya kampuni ya Emirates kutoka Umoja wa falme za kiarabu  hadi mjini New York ambako ilitua salama. Shirika la kijeshi la  Marekani na Canada, NORAD limesema lilikuwa na shaka  kwasababu ndege hiyo iliyokuwa na abiria 201 ilisafiri katika anga ya Canada  na  baadaye  kuingia   katika  anga ya Marekani. Ndege  mbili za kivita za Marekani ziliisindikiza ndege hiyo hadi katika uwanja wa ndege wa John F Kennedy nchini Marekani. Shirika la upelelezi la FBI limesema kuwa ndege hiyo ilikuwa na mizigo  kutoka Yemen.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Rtre/Afpe Mhariri:Sekione Kitojo