1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKIO: Wataalamu kuchunguza uharibifu kwenye mtambo wa nyuklia

5 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBc0

Tume ya wataalamu wa kinyuklia wa Umoja wa Mataifa,imewasili Japan kutathmini hali ya mtambo wa nyuklia ulioharibika vibaya sana katika tetemeko la ardhi la tarehe 16 mwezi Julai.Watu 11 walipoteza maisha yao na zaidi ya 1,000 wengine walijeruhiwa katika tetemeko hilo lililokuwa na nguvu ya 6.8 katika Kipimo cha Richter.Tetemeko hilo pia lilisababisha mtambo huo kuwa na kasoro kadhaa na kuvuja.Hali hiyo imezusha wasiwasi kuhusu usalama katika mitambo ya nyuklia ya Japan.

Kuanzia Jumatatu,tume ya Shirika la Nishati ya Kinyuklia la Umoja wa Mataifa IAEA,kwa muda wa siku nne,inatazamia kuuchunguza mtambo uliopata madhara.Siku ya Ijumaa tume hiyo itakutana na maafisa wa Kijapani wanaoshughulikia usalama wa nishati ya nyuklia.