1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo: Japan itafanya mazungumzo ya moja kwa moja na Korea Kaskazini

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCNu

Japan na Korea kaskazini zimetangaza mipango ya kukutana wiki ijayo mjini Hanoi kwa madhumuni ya kuyafanya mahusiano yao kuwa ya kawaida. Msemaji wa serekali mjini Tokyo amesema mkutano baina ya nchi hizo mbili hapo Machi 7 na 8 utajaribu kutanzua mivutano kuhusu kutekwa nyara raia wa Kijapani katika miaka ya sabini na ya thamanini. Serekali ya Korea Kaskazini imekiri kwamba iliwateka nyara raia 13 wa Kijapani na kuwarejesha watano kati ya hao miaka mitano baadae. Ilisema waliobaki walikufa. Hata hivyo, Japan inashikilia kwamba Korea Kaskazini huenda ikliwateka nyara watu zaidi, na baadhi yao bado wangali hai.