1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO:Japan kufanya jaribio la Kombora PAC-3 mwezi ujao

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUe

Japan imesema itafanya majaribio ya makombora yake ya kuzuia mashambulio ya adui mwezi ujao.

Mapema mwaka huu Japan ilipeleka makombora yake ya kwanza aina ya PAC- 3 katika eneo la Saitama nje ya Tokyo kwa madhumuni ya kujaribu kuimarisha ulinzi wake dhidi ya vitisho vya Korea Kaskazini.

Wizara ya ulinzi ya Japan inapanga kuleta kombora hilo aina ya PAC-3 mjini Tokyo kwa ajili ya kulifanyia majaribio.Kombora hilo linauwezo wa kwenda umbali wa kilomita 15 hadi 20.