1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO:Japan na Uchina kuimarisha uhusiano

12 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAc

Waziri Mkuu wa Uchina Wen Jiabao amenyoshea nchi ya Japan mkono wa urafiki ili kujaribu kumaliza tofauti zilizokumba nchi hizo mbili hapo awali.

Katika hotuba ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Uchina

Nchini humo katika kipindi cha miaka 22,Bwana Wen anashawishi nchi ya Japan kutosahau yaliyopita vilevile kutambua kuwa watu wake walikuwa wahanga wa vita.Kiongozi huyo alitembelea maeneo ya barabara za mji na kuwasalimu wakazi mjini Tokyo.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yaliyo na uchumi mkubwa zaidi barani Asia uliharibika katika kipindi cha miaka ya 2001 hadi 2006 wakati Waziri Mkuu wa Japan Junichiro Koizumi kuzuru makaburi ya vita mara kadhaa mjini Beijing na Seoul.

Uchina na Japan zinazidi kushirikiana kibiashara ingawaje uhusiano wao bado si mzuri.Japan inategemea wafanyikazi na wateja wa daraja ya katikati kutoka kwa Uchina.

Nchi ya Uchina ndiyo nchi pekee ya bara Asia iliyo na kura ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.