1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Toulouse: Kitisho cha migomo katika kampuni ya kutengeneza ndege ya Airbus

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCNx

Kampuni ya Ulaya ya kutengeneza ndege, Airbus, mwishowe leo itafichuwa mipango yake ya kujirekebisha, huku wafanya kazi wake wakivunjwa moyo, na kukiweko upinzani kutoka vyama vya wafanya kazi. Jana wafanya kazi katika kiwanda chake huko Kaskazini ya Ufaransa walisita kufanya kazi waliposikia tetesi kwamba idadi ya wafanya kazi itapunguzwa. Mjini Brussels, maafisa wa vyama vya wafanya kazi kutoka Uengereza, Ufaransa, Ujerumani na Spain wamekutana kuowanisha mikakati yao na kudokeza kwamba mgomo wa Ulaya nzima unaweza ukafanyika mnamo wiki chache zijazo.

Katibu Mkuu wa vyama vya wafanya kazi wa chuma katika Ulaya, Peter Scherrer, amesema:

+ Sisi tuko tayari kutafuta suluhisho na tuko tayari kufanya mazungumzo, lakini ikiwa mambo yatajitokeza kama vile tulivohofia, basi hapo tutajikusanya na kujipanga na matokeo yake ni kwamba katika baadhi ya sekta kutakuweko migomo.+

Hadi nafasi za kazi 10,000 zitaweza kupotea katika kampuni hiyo ya Airbus kutokana na mpango huo wa marekebisho utakaogharimu Euro bilioni tano.