1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Toure kushinda tuzo ya nne ya mchezaji bora?

27 Desemba 2014

Kiungo wa Cote d'Ivoire YayaToure ana nafasi kubwa ya kushinda kwa mara ya nne mfululizo Tuzo ya Mchezaji bora wa Mwaka Barani Afrika baada ya kujumuishwa katika orodha ya wagombea watatu wa mwisho

https://p.dw.com/p/1EAbn
Bildergalerie Afrikanische Fußballspieler Yaya Toure
Picha: Getty Images/A. Livesey

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang na kipa wa Nigeria Vincent Enyeama ndio wagombea wengine wanaoikodolea macho tuzo hiyo ya kifahari katika kandanda ya Afrika.

Toure anaichezea klabu ya Premier League ya England Manchester City ambayo ilishinda taji ligi msimu uliopita. Aubameyang anaichezea Borussia Dortmund ya Ujerumani wakati Enyeama akiendesha shughuli yake katika klabu ya Lille ya Ufaransa. Kura kutoka kwa makocha 56 wa kitaifa barani Afrika ndizo zitakazoamua mshindi, ambaye atatangazwa Januari 8 mjini Lagos.

Mshambulizi wa Cameroon Samuel Eto'o ameshinda taji hilo mara nne, lakini kati ya mafanikio hayo alishinda mara tatu mfululizo na wala siyo nne mfululizo. Abedi Pele pia aliitwaa tuzo hiyo mara tatu mfululizo…Toure alifunga mabao 20 katika mechi 35 za Premier League

Aubameyang aliisaidia BVB kumaliza wa pili katika Bundesliga msimu uliopita kwa kuwafungia mabao 13, ijapokuwa msimu huu mambo hayawaendei vyema ijana hao wa Kocha Jurgen klopp

Enyeama alikuwa na msimu mzuri na kuisaidia Lille kumaliza katika nafasi ya tatu katika Ligue I ya Ufaransa. Na lakini pia aliisaidia sana Nigeria katika Kombe la Dunia

Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka anayecheza soka yake barani Afrika itashindaniwa na wachezaji wa klabu ya Algeria ya Entente Setif, El-Hedi Belameiri na Akram Djahnit na Firmin Mubele wa V Club ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters/dpa
Mhariri: Mohammed Dahman