1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tripoli: Serekali ya Sudan inasitisha mapigano katika Darfur

28 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Bs

Mwanzoni mwa mazungumzo ya kutafuta amani ya mkoa wa Darfur yanayofanyika Libya hivi sasa, serekali ya Sudan imetangaza inasimamisha mapigano. Mkuu wa ujumbe wa serekali ya Sudan katika mazungumzo hayo, Nafie Ali Nafie, alisema amri hiyo inaanza kutoka sasa. Baadhi ya makundi ya waasi wa kutoka Darfur, ambayo mwanzoni yalisema yataususia mkutano huo, sasa yametangaza yako tayari kuzungumza na wapatanishi wa Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Afrika. Shirika la habarai la Kifaransa, AFP, limeripoti kwamba makundi mengine ya waasi wa Darfur yanashauriana juu ya kuwa na msimamo wa pamoja katika mkutano huo. Huko Darfur wanamgambo wa Kiarabu wanaosaidiwa na serekali ya Khartoum wanapigana na waasi wa Kiafrika. Tangu mwaka 2003 si chini ya watu laki moja wameuwawa na zaidi ya milioni mbili wamepoteza makaazi.