1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tripoli yazidi kushambuliwa

Halima Nyanza(ZPR)17 Julai 2011

Milipuko mikubwa imesikika mfululizo, mapema leo katika mji mkuu wa Libya Tripoli, uliongome ya kijeshi ya kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.

https://p.dw.com/p/11wpu
Mji wa Tripoli washambuliwa zaidiPicha: dapd

Milipuko 13, ilisikika jana usiku na mapema leo asubuhi. Hata hivyo haikuelezwa mara moja nini lengo la milipuko hiyo.

Lakini kituo cha Televisheni cha taifa cha Al Jamahiriya kimeripoti kwamba Majeshi ya NATO yameshambulia maeneo ya raia na yale ya kijeshi katika maeneo ya Ain Zara na Tajoura, mashariki ya Tripoli.

Tripolis Gaddafi Libyen Luftangriff NATO
Baadhi ya majengo yaliyoharibiwaPicha: picture alliance/dpa

Kituo hicho, kilinukuu duru za kijeshi, kwa kusema kuwa kuna watu walioathiriwa na mashambulio hayo, lakini hakikutoa taarifa kamili.

Wakati huohuo waasi 10 wa Libya wameripotiwa kuuawa na wengine 172 wamejeruhiwa katika shambulio lililofanywa jana katika mji wa magharibi mwa nchi hiyo wa Brega, wakati waasi hao wakiendelea mbele na mapambano kwa kuwarudisha nyuma wanajeshi wa Gaddafi.