1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump akubali kuwa mgombea wa Republican

22 Julai 2016

Mgombea wa chama cha upinzani cha Republican nchini Marekani Donald Trump amehitimisha mkutano mkuu wa siku 4 wa chama chake mjini Cleveland kwa kuwahutubia maelfu ya wafuasi wa chama hicho

https://p.dw.com/p/1JU4R
USA Republican National Convention in Cleveland Donald Trump Rede
Donald Trump akihutubia ClevelandPicha: picture-alliance/dpa/S. Thew

Zingaito la hutuba yake likiwa matatizo ya ajira, usalama, uhamiaji na wakimbizi na mgogoro wa muda mrefu wa Mashiriki ya Kati kuwa ni matokeo ya utawala usiojali watu wake wa chama cha Democratic huku akitoa ahadi ya utawala utakaozingatia sheria.

Donald Tramp alianza kwa kupokea kwa heshma uteuzi wa chama chake cha Republican katika kuwania nafasi ya rais mwezi Novemba mwaka huu na kuanisha dira ya mipango yake ya maendeleo endapo atachaguliwakuwa rais wa taifa hilo. Amesema angependa kuitanguliza mbele Marekani hasa katika kuingia katika makubaliano ya kibiashara na kusitisha uhamiaji haramu.

Mbele ya umati mkubwa wa wafusia wa chama chake amemshambulia mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton kwa uamuzi wake wakati akiwa waziri wa mambo ya kigeni kwa mpango wa nyuklia wa Iran na mzozo Mashariki ya Kati.

USA Republican National Convention in Cleveland Donald Trump Rede
Wafuasi wa chama cha RepublicanPicha: Reuters/C. Allegri

Kauli kali ya Trump

"Iraq ipo katika machafuko, Iran ipo katika kuunda silaha za nyuklia, Syria imegeuka kuwa magofu kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, mgogoro wa wakimbizi hivi sasa umekithiri vibaya, baada ya miaka 15 ya vita katika Mashariki ya Kati, baada ya matumizi wa matrilioni ya dola na kupotea kwa maelfu ya watu hali imekuwa mbaya katika kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa. Hii ndio kumbukumbu aliyoiacha Hillary Clinton, vifo, maangamizi, ugaidi na udhaifu." Alisema Trump.

Aidha mgombea huyo hakuacha kumlaumu Rais Barack Obama kutokana na mauwaji yaliyotea katika siku za hivi karibuni yanayohusisha raia na polisi nchini humo akitaja idadi ya polisi waliouwawa wakiwa madarakani imeongezeka kwa asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

"Mji ambao anatoka rais, Chicago, zaidi ya watu 2,000 wameathiriwa na mashambulizi ya bunduki kwa mwaka huu pekee. Na karibu watu elfu 4 wameuwawa katika mji huo tangu aingie madarakani." Alisema Trump.

Suala la uhamaji

Akizungumzia wimbi la uhamiaji amesema karibu watu laki moja na elfu themanini, wahamiaji haramu wenye rekodi za uhalifu wanaonigia katika ardhi ya nchi hiyo wamekuwa huru kabisa na kutishia usalama wa raia. Kutokana na hali hiyo amesema atakata mahusiano na mataifa yenye kujifungamaisha na ugaidi na kujenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico kukatisha makubaliano ya kibiashara na mjadala wake kuanza upya.

Kwa nje ya mipka hiyo hotuba ya Trump imeikosoa China kwa kusema inafanya vitendo vya wizi wa haki za wamiliki ubunifu na kufanya ulaghai wa nguvu ya sarafu yake jambo ambalo ameahidi kuwa atalisimamisha endapo ataingia madarakani.

Lakini baadhi ya watu wameanza kutoa maoni yao kuhusu hotuba hiyo. Aliyekuwa mgombea tiketi ya urais kwa upande wa Democratic Bernie Sanders katika ukurasa wake wa Twitter alinukuu kauli ya Trump ya majingambo iliyosema hakuna anayeujua mfumo wa nchi hiyo zaidi yake na kusema peke yake anaweza kuweka mambo sawa akihoji mgombea huyo anawania urais wa udikteta? Lakini Dayna Dent kutoka Washington alisema Trump si mtu anayeiga na anampenda sana.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP/APE
Mhariri:Josephat Charo