1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRUVADA kinga ya maambukizi UKIMWI

11 Mei 2012

Nchini Marekani, dawa ya kwanza kuonyesha udhabiti wa kupambana na maambukizi ya Virusi vinavyosababisha UKIMWI imeruhusiwa kutumiwa kwa watu walio katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.

https://p.dw.com/p/14tlp
Miongoni wa mabango ya UKIMWI
Miongoni wa mabango ya UKIMWIPicha: AP

Vidonge vya Truvada ambayo vilionyesha udhabiti huo tangu mwaka 2004 baada ya Taasisi ya sayansi ya Gilead, yenye makao yake makuu Foster, CCalifornia, Marekani, kufanya utafiti kwa kuunganisha dawa mbili za kupambana na ugonjwa huo za awali EMTRIVA na VIREAD.

Familia ya Baba, mama na mtoto
Familia ya Baba, mama na mtotoPicha: AP

Kuruhusiwa kwa tembe hiyo kunatokana na kikao maalumu cha Bodi ya ushauri ya Chakula na Dawa nchini Marekani kufikia maamuzi hayo yaliyochukua saa12 na kukubaliwa, lakini tamati ya yote itakuwa Juni 15.

Dawa ya TRUVADA inaweza kuwasaidia watu wanaoishi pamoja wakati mmojawapo wa mpenzi amekwisha ambukizwa ugonjwa huo, na kumsadia mwenzake mzima kutoambukizwa ugonjwa huo.

Uwezo wa dawa hii kuzuia umeonekana kwa asilimia 75 kwa mmojawapo wa wapenzi, akiwa tayari ameabukizwa; hii ni katika utafiti uliofanyika mwaka jana. Lakini uthabiti wake ni kwa asimilia 42 tu, kwa wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Wale walio katika mazingira hatari wanatakiwa kumeza dawa hizo kila siku, lakini inawekwa wazi kuwa dawa hiyo haimsadii kabisa mtu ambaye amekwisha ambukizwa ugonjwa wa UKIMWI, kwani kama akijaribu kutumia dawa ya TRUVADA basi anaweza kuwa katika hatari ya kushindwa kabisa kupata afueni baada ya kutumia tembe hizi.

Dr Tom Giordano ambaye ni miongoni mwa wanaounga mkono matumizi ya tembe hizo, na aliunga mkono dawa hiyo kuanza kutumika, amesema bayana kuwa watu ambao hawajapima kuwa wameambukizwa ni vema kupima na kujua hali zao kabla ya kuanza matumizi .

Gharama ya tembe za TRUVADA

Lakini changamoto kubwa ya dawa hii ya TRUVADA ni kuuzwa kwa gharama kubwa na kuweza kuwafikia kila watu walio katika mazingira ya hatari sana kwani vidonge kwa matumizi ya mwezi mmoja vinauzwa dola 900, na matumizi kwa mwaka mzima sawa na dola11,000 za Kimarekani.

Gharama ya vidonge hivyo kwa mtu mmoja kwa mwezi inalinganisha sawa na gharama ya kuwahudumia wagonjwa 20 wenye maambukizi ya UKIMWI.

Tabibu akiwa kazini
Tabibu akiwa kaziniPicha: AP

Nchini Marekani kwa sasa kuna watu wenye virusi vinayoambukiza UKIMWI wanaofikia milioni 1.5, huku maambukizi kwa sasa ni watu 50,000 kwa mwaka mmoja tu. Mpaka sasa tiba ya ugonjwa wa UKIMWI bado haijapatikana, huku watu zaidi ya 240,000 nchini humo wameambukizwa UKIMWI, lakini hawajui kuwa wana Virusi hivyo.

Mwandishi:Adeladius Makwega

Mhariri: Othman, Miraji