1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tsunami yaua wengi Indonesia.

Halima Nyanza(ZPR)27 Oktoba 2010

Watu 112 wamefariki dunia na wengine zaidi ya mia tano hawajulikani walipo, baada ya kimbunga cha tsunami kukikumba kisiwa cha Mentawai, kilichoko kilomita 150 magharibi mwa pwani ya Sumatra nchini Indonesia.

https://p.dw.com/p/Poj4
Mlima Merapi nchini Indonesia, ambao volcano ililipuka.Picha: picture-alliance/dpa

Kimbuka hicho cha tsunami iliyofikia urefu wa mita tatu, kimekuja dakika chache baada ya tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo siku ya Jumatatu.

Nyumba kadhaa zimeharibiwa kutokana na mawimbi hayo yaliyofika mita 600 katika nchi kavu.

Indonesien Vulkanausbruch Merapi
Wanavijiji walioyahama makaazi yao, kutokana na kulipuka kwa volcano katika mlima Merapi.Picha: AP

Wakati huohuo watu 25 wamekufa baada ya mlima Merapi nchini Indonesia kulipuka mara tatu jana.

Hatua hiyo ilisababisha, maelfu ya watu kuyahama makaazi yao.