1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tuhuma za wizi wa watoto Haiti

1 Februari 2010

Wamerekani 10 wamekamatwa kutokana na kutuhumiwa kuwa na mpango wa kuwaiba watoto nchini Haiti. Inadaiwa kwamba wamarekani hao kutoka kanisa la Kibaptisti walikuwa wanakusudia kuwaiba watoto 33. Lakini wamekanusha

https://p.dw.com/p/LoZ7
Mayatima wa HaitiPicha: AP

Wamarekani hao 10 waliotiwa ndani waliokuwa wanataka kuwatoa watoto hao nje ya Haiti,wamesemakuwa walikuwa wanajaribu kufanya jambo sahihi kwa kutekeleza misingi ya dini ya ukristo, kwa kuwaokoa watoto.Waziri Mkuu wa Haiti Max Bellerrive ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba watu hao walikamatwa jana na sasa wanafanyiwa uchunguzi.

Hatahivyo wamerekani hao wamekanusha tuhuma hizo na wameeleza kuwa walikuwa wanakusudia kuwapeleka watotoa hao kwenye nyumba ya yatima katika nchi jirani ya Jamhuri ya Dominic-walikamatwa walipokuwa wanajaribu kuwatoa watoto hao 33 kwa basi na kuwapeleka katika jamhuri ya Dominic.

Licha ya kukanusha madai ya kuwaiba watoto hao msemaji wa wamarekani hao amekiri kwamba hawakuwa na kibali kutoka kwa wahusika wa Haiti.

Msemajji huyo Luara Silsby ameeleza''Watoto hawa wamepoteza makaazi na familia zao na sasa wanahitaji sana mapendo yote ya mwenyezi Mungu na rehema zake na wanahitaji mahali pa kulelewa."

Bila vibali

Mkuu wa shirika la kuwasaidia watoto nchini Haiti, Patricia Vergas amesema idadi kubwa ya watoto hao bado wana ndugu ambao wapo hai.Waziri wa ustawi wa jamii nchini Haiti Yves Christallin alisema palikuwa na tuhuma kwamba Wamarekani hao walikuwa wanataka kuwapeleka watoto hao kwa wazazi wa hiari.

Lakini msemaji wa shirika ,la wamarekani hao la hifadhi ya watoto Children's Refuge kutoka jimbo la Idaho bibi Silby amekanusha tuhuma hizo

Juu ya maelezo yaliyotolewa na msemaji huyo, kwamba shirika lake lilikuwa na dhamira ya kuwasaidia watoto wa Haiti,msemajiwa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto Unicef Bwana Kent Page ameeleza''Pana taratibu zinazopaswa kufuatwa.Mtu hawezi kujichukulia mtoto tu, na kuondoka naye-kwa kweli haiwezekani hata ikiwa mtu huyo anakusudia kutenda mema".


Wazazi wa hiari

Haiti UNICEF Notunterkunft
Mayatima wa Haiti kwenye nyumba moja Port-Au-PrincePicha: AP

Wamarekeni hao 10 ni watu wa kwanza kukaamatwa tokea Haiti ikumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi.Kwa mujibu wa takwimu rasmi watu mia moja na sabini alfu wamekufa kutokana na tetemeko hilo. Watoto wengi wamepoteza wazazi wao.Na kutokana na hali hiyo serikali ya Haiti imetahadharisha juu yao uovu wa kuibiwa kwa watoto nchini humo. Mkurugenzi wa taasisi ya ustawi wa jamii Jeanne-Bernard Pierre amesema taasisi yake imepata habari juu ya kuondoka nchini kwa watoto bila ya ruhusa.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa watoto hao 33 pamoja na wamarekani 10 walisi mamishwa kwenye mpaka na Jamhuri ya Dominic.Wamerakani hao hawakuwaambia maafisa wa uhamiaji kwamba walikuwa wanawatoa watoto nje ya nchi. Amesema ni wakati wa kufanya ukaguzi kwamba afisa mmoja wa polisi aligundua kwamba watoto kadhaa waliokuwamo ndani ya basi hawakuwa na hati za kusafiria.

Wakati huo huo Ikulu ya Marekani imesema jeshi la nchi hiyo litaanza tena kuwasafirisha kwa ndege kuwapeleka Marekani watu waliokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi na kuwapatia matibabu nchini .Marekani.Jeshi la Marekani liliusimamisha mpango huo Jumatano wiki jana.

Mwandishi Mtullya Abdu.ZA/AFPE

Mhariri/...Mwadzaya Thelma