1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TURIN:Katibu mkuu wa umoja wa mataifa aelekea Sudan

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTD

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon leo yuko njiani kuelekea nchini Sudan katika ziara yenye lengo la kuanzisha hatua ya kwanza ya mkakati wa kutafuta suluhisho la kumaliza mzozo katika jimbo la Darfur kwa njia ya mazungumzo na pia kupelekwa wanajeshi wa kulinda amani katika eneo hilo.

Katibu mkuu ametokea katika mji wa Turin nchini Italia ambako alikutana na maafisa wakuu wa umoja wa mataifa.

Bwana Ban Ki Moon anatarajia kuuwasilisha mpango wake huo kwa rais Omar Hassan el Bashir wa Sudan.