1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tusker ni mabingwa wa Afrika mashariki na kati.

28 Julai 2008

Tusker wameipiga kumbo mjini Dar-es-salaam, TUgandan revenue Authority na kutwaa ubingwa.

https://p.dw.com/p/ElQp

Tusker ya kenya ni mabingwa wapya wa kombe la Kagame-kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika mashariki na kati na kwanini young Africans ya Tanzania iligoma kuteremka uwanjani na Simba kuania nafasi ya 3 ?

Barcelona,itayari kumbadilisha stadi wa Kamerun Samuel Eto'o kwa Karim Benzema na mabingwa wa Ufaransa Olympique Lyon.

Wakati wenyeji Beijing wanaandaa jumamosi hii ijayo majaribio ya sherehe za ufunguzi wa michezo ya Oliompik ya Beijing hapo August 8, stadi na matumaini ya Kenya kwa medali ya dhahabu katika mita 800 Pamela Jelimo,ataka medali hiyo ya dhahabu kkumfuta machozi mama yake.

►◄

Tukianza na dimba, mabingwa wapya wa kombe la Kageme-kombe la klabu-bingwa kanda ya Afrika mashariki na kati limeenda mara hii Kenya.Tusker iliitimua Ugandan Revenue Authority jana na kutwaa kombe.

Young Africans ya Tanzania iliokua ikumbane na mahasimu wao simba jumamosi- hawakuonekana uwanjani -kisa nini ?

Young Africans hawakushuka uwanjani kwa dai kwamba walitaka walipwe kitita cha Tsh. milioni 50. CECAFA haikulikubali ombi hilo na Yanga huenda ikaadhibiwa.

Tukisalia katika medani ya dimba, FC Barcelona ya Spain, imeridhia kubadishana stadi wa simba wa nyika -Kamerun, Samuel Eto'o na stadi wa Olympic Marseille,mabingwa wa Ufaransa-Karim Benzema-hii ni kwa muujibu wa gazeti la kila siku la michezo la Catalan.

Sport likaarifu kwamba ,Lyon ina hamu ya kumfungisha mkataba Eto'o ambae hatakiwi na kocha mpya wa Barcelona , Josep Guardiola. Barcelona kwa miezi kadhaa imekua na hamu ya kumuajiri Benzema.

Washambulizi wengine ambao Barcelona ina hamu sana kuwaajiri ni Muivory Coast,Didier Drogba wa chelsea, Emannuel Adebayor wa Arsenal na David Trezeguet wa Juventus.

Stadi wa zamani wa timu ya taifa ya ujerumani Pierre Litbarski,maarufu kwa chenga zake za ajabu anakuwa kocha mpya wa klabu ya Iran ya SAIPA TEHERAN.

Mkataba wa mwaka mmoja na litbarski, umetiwa saini nchini Uturuki ambako Saipa imeingia katika kambi ya mazowezi.

Litbarski amekuwa miaka mingi japan akiifunza timu ya Fukuoka na anachukua wadhifa wa Ali Dae anaekuwa sasa kocha wa timu ya Taifa ya Iran.

Saipa Teheran, waliibuka mabingwa mwaka ja na 2007 na wameingia robo-finali ya kombe la klabu bingwa barani Asia.

MICHEZO YA OLIMPIK YA BEIJING itafunguliwa rasmi August 8 kiasi cha siku 11 kutoka leo.wanariadha wake kwa waume, wameshaanza kuwasili katika kijiji cha Olimpik.Wa kwanza kabisa walikuwa wanariadha China.Hata kikosi cha Ujerumani kimewasili Beijing na kuingia kwenye kijiji hicho .

Kiongozi mmoja wa kikosi cha Ujerumani kilichowasili mwishoni mwa juma katika kijiji cha olimpik alitoa sifa hizi kwa kijiji hocho:

"Bila shaka kijiji hiki ni kimoja kati ya vile vizuri kabisa niliojionea hadi sasa.Kila unapokwenda kuna vidimbwi vya maji,miti na mandhari ya kijani na inapendeza sana, sana."

Wakati ufunguzi rasmi wa michezo hii utakua tarehe 8 mwezi wa 8 mwaka 2008, jumamosi ijayo kutafanyika majaribio ya sherehe zenyewe za ufunguzi kabla ya siku yenyewe ambapo hadi viongozi wa dola na serikali 80 watahudhuria pamoja nao rais George Bush wa Marekani na Nicholas Sarkozy wa Ufaransa.

Waandazi wa michezo hii walikanusha hapo kabla taarifa zilizodai kwamba mazowezi yaliopangwa ijumaa na jumamosi iliopita yalivunjwa dakika ya mwisho kutokana na hofu za hujuma ya kigaidi kutokea.

Miongoni mwa wanariadha wanaotazamiwa kutamba Beijing, ni msichana chipukizi wa Kenya, mwenye umri wa miaka 18 : Pamela jelimo.

Jelimo ameusangaza msimu wa riadha wa mwaka huu kwa jinsi alivyotia fora katika mbio za masafa ya mita 800 na kumpiku mkenya mwenzake bingwa wa dunia Jenneth Jepkosgei.

Pamela anasema uchu wake wa ushindi huko Beijing unatokana na kumfurahisha mama yake Rodah Jeptoo Keter,ambae maisha yake ya riadha yalimalizika haraka kwa kubidi kufunga ndoa na mapema.

Jelimo amearifu kwamba, mama yake aliekuja kuzaa watoto 9,yeye akiwa 4 atafurahi sana kumuona yeye anafanikiwa katika m chezo ambao yeye mama yake alishindwa kufaulu.

Kama mama yake, jelimo alianza kukimbia mbio za masafa ya mita 400 katika shule ya msingi ya Koyio huko Rift Valley,lakini alianza kukimbia masafa ya mita 800 hapo April mwaka huu.Kiroja cha mambo alitiwa shime na shoga yake anaefanya nae mazowezi bingwa wa dunia wa Osaka, Jeneth Jepkosgei, aliekuwa mkenya wa mwanzo mwanamke kuvaa taji la ubingwa wa dunia katika masafa hayo.Na sasa Jelimo amempiku Jeneth.

Macho ya Kenya na afrika nzima yanakodolewa sasa kwa wasichana hao 2 wanavaa kiatu kilichoachwa na mwanamsumbiji Maria Mutola, bingwa mara kadhaa wa dunia na Olimpik huko sydney, 2000.

Tumalizie, mbio za baiskeli za Tour de France: Spian imetoroka na taji lake la 3 kubwa la kispoti-baada ya kombe la ulaya la dimba, taji la tennis la wimbledon na jana la mbio za baiskeli za Tour de France.

Mspain Carlos Sastre ndie bingwa wa 2008 wa tour de France.