1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tuzo la Nobel la Amani

11 Desemba 2010

Liu Xiabo ametunukiwa tuzo la Nobel la amani.

https://p.dw.com/p/QVnx
Mwenyekiti wa kamati ya Nobel Thorbjoern Jagland,ameketi karibu na kiti kitupu katika sherehe za kumtuza Liu Xiaobo (kwenye picha iliyoangikwa).Picha: AP

Mwanaharakati  raia  wa  China  ambaye  yuko  kifungoni   Liu Xiabo ametunukiwa tuzo ya  amani  ya Nobel  katika sherehe ambazo hakuhudhuria na badala yake palikuwa na kiti kitupu na picha yake.

Akiwa gerezani anakotumikia kifungo cha miaka 11, Liu alisema tuzo hiyo iwaendee waliofariki mnamo mwaka 1989 katika uwanja wa Tiananmen.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Nobel,Thorbjorn Jagland ametoa wito wa kuachiliwa  Liu  haraka.

Norwegen China Friedensnobelpreis Verleihung an Liu Xiaobo in Oslo Flash-Galerie
Stashahada ya Nobel ya Liu Xiabo.Picha: AP

Serikali ya China haikumruhusu yeyote aliye na uhusiano na Liu kwenda Oslo na imelitaja tuzo hiyo kuwa udanganyifu wa kisiasa. China inaonekana kuzuwia mitandao ya habari ya nchi za magharibi, na vyombo vya habari vya taifa havikuzitaja sherehe hizo isipokuwa kutoa taarifa ya kushutumu tuzo hiyo.

Kilele cha sherehe hizo kilikuwa ni maandamano ya kuwasha mwenge mjini Oslo.

Mwandishi:Maryam Abdalla/Rtre

Mhariri:Sekione Kitojo.