1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tuzo ya DW ya Uhuru wa Kutoa Maoni

21 Aprili 2016

Mhariri mkuu wa gazeti linalosomwa na wengi nchini Uturuki,"Hürriyet" ametunukiwa tuzo ya Deutsche Welle ya uhuru wa mtu kutoa maoni yake.Mkurugenzi mkuu wa DW Peter Limburg amemsifu Sedat Ergin na kusema aanastahiki

https://p.dw.com/p/1IaO7
Nembu ya Tuzo ya DW ya Uhuru wa mtu kutoa maoni yakePicha: DW/M.Müller

Sedat Ergin anakabiliwa hivi sasa na mashitaka kwa makosa ya kumtukana rais. Chanzo ni ripoti yake iliyochapishwa mwezi wa Septemba ambapo aliikosoa hotuba iliyotolewa na rais Reccep Tayyip Erdogan. Ofisi za gazeti lake "Hürriyet, zilivamiwa mara mbili msimu wa mapukutiko mwaka jana na wafuasi wa chama cha kihafidhina cha kiislam cha rais Erdogan. Sedat Ergin anakumbwa na kishindo kile kile kinachowakumba mamia kadhaa ya waandiishi habari nchini Uturuki. Miezi iliyopita mhariri mkuu wa gazeti linaloikosoa serikali,Jumhuriyat, Dschann Dündar na mwenzake Erdem Güll walikamatwa kutokana na amri ya rais Erdogan.

Sedat Ergin ni mshindi mstahiki anasema mkurugenzi mkuu wa DW Peter Limbourg

Akimtunukia tuzo hiyo Sedat Ergin,kiongozi mkuu wa DW Peter Limbourg amesema:"Sedat Ergin ni mshindi mstahiki wa tuzo hii. Anapigania uhuru wa vyombo vya habari,anakabiliwa na vitisho nchini Uturuki na nnaamini ,sisi kama Deutsche Welle hatuwezi tena kuvumilia kuona waandishi habari,wataalamu, na wasanii nchini Uturuki wakiandamwa na viongozi wa Uturuki. Na ndio maana,naamini hii ni ishara ya maana kutoka Ujerumani pia kwamba hatutovumilia tena mitindo kama hiyo pamoja na kutoheshimiwa uhuru wa mtu kutoa maoni yake."

Peter Limbourg
Mkurugenzi mkuu wa Dw Peter LimbourgPicha: DW

Mhariri mkuu wa gazeti la Hüriyet Sedat Ergin ameshukuru kwa kutunukiwa tuzo ya mwaka huu ya DW ya uhuru wa mtu kutoa maoni yake.

Haijulikani bado kama Sedat Ergin atafika Bonn kuüpokea tuzo hiyo

Haijulikani bado kama Sedat Ergin binafsi atapokea tuzo hiyo wakati wa Kongamano la Vyombo jumla vya habari linaaloandaliwa kila mwaka na DW. Mwaka huu kongamano hilo litafanyika mwezi ujao wa juni.Tangu mwezi Machi uliopita mwandishi habari huyo anashitakiwa kwa makosa ya kumtusi rais Erdogan.

Bobs Award Freedom of Speech Sedat Ergin
Mhariri mkuu wa gazeti la Hürriyet Sedat ErginPicha: privat

Tuzo ya DW ya uhuru wa mtu kutoa maoni yake imeanza kutolewa mwaka 2015 kama sehemu ya shindano la "mwanaharakati bora katika mtandao"The Bobs-Best of Online Activism."Wanaotunukiwa tuzo hiyo ni watu mashuhuri wanaopigania kwa kila hali haki za binaadam na uhuru wa mtu kutoa maoni yake.Tuzo ya kwanza alitunukiwa mwaka jana mwanabologi wa Saudi Arabia Raif Badawi. Na kwakuwa mwenyewe yuko gerezani,mkewe Ensaf Haidar ndie alikaebidhiwa tuyo huzo kwa niaba zake.

Mwandishi: Koch Martin&Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Gakuba Daniel