1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tuzo ya uhuru wa vyombo vya habari , Merkel amtunza mchoraji wa Denmark Westergaard

Sekione Kitojo9 Septemba 2010

Jioni ya jana katika mji wa Potsdam kulifanyika hafla ya kumpa tuzo msanii wa vibonzo kutoka Denmark Kurt Westergaard, tuzo ya vyombo vya habari.

https://p.dw.com/p/P7cg
Mchora katuni kutoka Denmark Kurt Westergaard akiwa na kansela wa Ujerumani Angela Merkel (CDU) baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya vyombo vya habari mjini Potsdam.Picha: AP

Katika  kasri  la  Sanssouci  mjini  Potsdam, usiku wa  jana  kulifanyika   hafla  ya  kumpa  tuzo  msanii  wa katuni   kutoka  Denmark  Kurt  Westergaard, tuzo  ya vyombo  vya  habari. Tuzo  hiyo  ilitolewa  na   kansela  wa Ujerumani  Angela  Merkel. Westergaard  alichora  moja kati  ya  vobonzo  12  vinavyomkejeli  mtume  Muhammad , ambapo  miaka  mitano  iliyopita  vilichapishwa  katika gazeti  la  Denmark  la  Jyllands-Posten.  Kibonzo alichokichora  kinaonyesha   mtume  Muhammad  akiwa  na bomu  katika  kilemba  alichovaa. Kuchapishwa  kwa vibonzo  hivyo  katika  mwaka  huo 2005  kulichochea ghasia   duniani  kote  katika  ulimwengu  wa  Waislamu  na kusababisha   maandamano  ya  ghasia.  Raia  huyo  wa Denmark  amepata  tuzo  hiyo  kwa   kutambua  mchango wake  katika  uhuru  wa  vyombo  vya  habari.

Baraza  la  ushauri  la   chama  cha  waandishi  habari   wa Potsdam   lilitaka  kuepusha  hatari,  na  kuzuwia  taarifa hizo  , na  kutangaza  siku  ya  tarehe  6.9, Jumatatu, mshindi  wa  tuzo  hiyo  kwa  mwaka  huu  2010,  kuwa  ni mchora  vibonzo  raia  wa  Denmark  Kurt  Westergaard, kutokana  na  msimamo  wake  usio  yumba   kwa  ajili  ya vyombo  vya  habari  na  uhuru  wa  mawazo  pamoja  na ushujaa  wake  wa   kulinda  thamani  ya   demokrasia licha  ya  ghasia   na  vitisho  vya  kuuwawa.

Westergaard,  anayeishi  hadi  sasa  katika  ulinzi  wa polisi  tangu  pale   vibonzo  hivyo  vilipochapishwa, hakutaka   kujiweka  katika  hatari  katika  hafla  hiyo  mjini Potsdam. Kwa  hiyo  kasri  hilo  la  Sanssouci  liliwekewa ulinzi  mkali  na  shughuli  ya  kukabidhi  tuzo  hiyo ilifanyika  katika  hali  ya  ulinzi  mkali.

Mwanachama  wa  chama  cha  waandishi  habari   wa Potsdam  na  mhariri  mkuu  wa  gazeti  linalosambazwa kwa  wingi  nchini  Ujerumani   la  Bild, Kai Diekman alikuwa  na  haya  ya  kusema.

Nadhani  hapa  sio  suala  la  hatari  ya  usalama,  hili  ni suala  la  udhibiti  wa   kimbinu, ndio  sababu  kuna  hali kama  hii,  ni  ishara  ya  kwamba  kile  ilichokisababisha katuni  hizo  hakikuleta  hali  nzuri. Na  mtu  hapaswi kuweka  msisitizo  zaidi.

Gazeti  la  Bild  kwa  mfano  liliamua  wakati  ule, kutochapisha  vibonzo  hivyo. Lakini  kile  kilicho  muhimu kwetu  sisi, ni  kwamba  tuko  katika  bara  la  Ulaya  na kwamba  sheria  lazima  zifuatwe .

Ameongeza   kuwa  hakubaliani  na  yeyote  atakayeeleza tofauti  na  hivi. Lakini  yuko  tayari  kutoa  maisha  yake kwa  kile  mchoraji  alichoweza  kukisema.

Na  msimamo  huo  umeonekana  katika  hafla  ya  jioni  ya jana.

Hotuba  kuu  ilitolewa   na  kansela  wa  Ujerumani  Anfela Merkel  katika  halfa  hiyo  mjini  Potsdam. Hotuba  yake ilisisitiza    zaidi   kuhusu  uhuru  wa  vyombo  vya  habari na  uhuru  wa  kutoa  mawazo.  Na  amemtetea  sana Westergaard. Kama  mchoraji  alipaswa   kufanya  kazi yake.

Haijalishi  iwapo  vibonzo  vyake  tunavipenda  ama   la, iwapo  tunapaswa   na   kwamba  tunamsaidia  ama hapana.  Ana  weza   kufanya  hivyo? Ndio anaweza. Yeye ni  msanii ,  kama   walivyo  wengi  katika  bara  la  Ulaya. Ulaya  ni  mahala  ambapo  msanii  anaruhusiwa  kueleza chochote. Hakuna  kitu  kinacholeta  mgongano, kwamba Ulaya  ni  mahali  ambapo  uhuru  wa  kuabudu  na  wa dini  unaheshimiwa  sana.

Wakati  huo  huo,  kiongozi  wa   baraza  kuu  la  Waislamu nchini  Ujerumani  Nadine  Elyas  amekosoa  hatua  hiyo ya  kumpa  tuzo  msanii  huyo  wa  kuchora  vibonzo.

Chama  cha  waandishi  habari  wa  Potsdam  kinatoa  tuzo hiyo   kila  mwaka  katika  mtazamo  wa  Ulaya  na  dunia, katika  kusisitiza  na  kuacha  alama  za  uhuru  wa  habari.

Mwandishi :  Wagner, Jörg / ZR / Sekione  Kitojo

Mhariri : Mohammed  Abdul Rahman.