1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tyson Gay atamba pia katika mita 200

Ramadhan Ali30 Agosti 2007

Mashindano ya riadha ya dunia yakiendelea huko Osaka,Japan ,Ujerumani imejipatia leo medali yake ya pili ya dhahabu wakati muamerika Tyson Gay ametamba katika mita 200.

https://p.dw.com/p/CHb7
Mjerumani Franka Dietzsch amenyakua medali ya dhahabu
Mjerumani Franka Dietzsch amenyakua medali ya dhahabuPicha: AP

Katika mashindano ya riadha mjini Osaka,Japan,muamerika Tyson Gay, ametoromka hivi punde na medali yake ya pili ya dhahabu-mara hii katika mita 200 akiongezea ile ya mita 100.Ujerumani imenyakua nayo medali yake ya pili ya dhahabu mara hii katika kurusha nyundo ikilwetwa na Betty Heidler.

Katika changamoto kabla ya finali ya mita 5000,bingwa wa dunia Eluid Kipchoge kutoka Kenya amempelekea salamu muethiopia Sileshi Sihine kwamba amekusudia kurudi tena Kenya na medali nyengine ya dhahabu .

Tyson Gaya yuko njiani kutimiza shabaha yake ya kurejea Marekani na medali 3 za dhahabu baada ya ushindi wake jinni hii katika mita 200 wanaume.Fay alichukua muda wa sek.19.76 kutimiza shabaha hiyo nadra ya mataji yote 2-mita 100 na 200.Mjamaica Usain Bolt alibidi kuridhika na medali ya fedha huku ile ya shaba ikienda pia Marekani kwa Wallace Spearmon.

Mpanama Irving Saldano alihitaji rekodi ya Marekani nzima katika kuchupa long jump ili arudi Panama na medali ya kwanza ya dhahabu.

Akichupa mara ya mwisho kabisa, Saldinho alichupa mita 8.57.Medali ya fedha ikaenda kwa bingwa wa Ulaya Andrew Howe wa Itali wakati ile ya shaba ikachukuliwa na muamerika Dwight Philips,bingwa wa 2005.

Msichana wa Ujerumani Betty Heidler ,ameipatia ujerumani leo medali yake ya pili ya dhahabu kutoka michezo hii.Alirusha nyundo masafa marefu zaidi kuliko bingwa wa dunia wa 2001 na 2003 Yipsi Moreno.Betty,alihitaji mita 74.76 kunyakua medali yake ya dhahabu.

Nae muastralia Jana Rawlinson, amenyakua medali yake ya pili ya dhahabu katika mbio za mita 400 kuruka viunzi kwa kumpita bingwa wa rekodi ya dunia kutoka Russia Yuliya Pechonkina.

Changamoto ya finali ya mita 5000 wanaume itakua tena kinyan’ganyiro kati ya majirani 2-Kenya na Ethiopia:Paka hayupo,panya hutawala.

Kenenisa Bekele mshindi wa mita 10.000 kutoka Ethiopia akiwa amezikwepa mita 5000,kinyan’ganyiro ni kati ya bingwa wa dunia mkenya Eluid Kipchoge na makamo-bingwa wa dunia katika mita 10.000 Sileshi Sihine wa Ethiopia.Katika mbio kabla ya finali hii leo, ilikua Kipchoge aliechukua muda bora.Sihine amempa Kichoge salamu kwamba kutangulia leo sio kufika kesho- siku ya finali.