1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majaji wa ICC, leo watatoa hukumu kusu Rais Bashir

Sudi Mnette
6 Julai 2017

Majaji wa Korti ya kimataifa ya Uhalifu ICC, leo watatoa hukumu juu ya kama Afrika Kusini ilikiuka sheria za ICC kwa kushindwa kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa ziara yake mjini Johannesburg mwaka 2015.

https://p.dw.com/p/2g33T
Äthiopien Gipfel Afrikanische Union - Omar al-Bashir
Rais Omar al-Bashir wa SudanPicha: Getty Images/AFP/T. Karumba

Hukumu ya leo itafuatiliwa kwa karibu kutokana na madhara inayoweza kuwa nayo kwa Bashir na viongozi wengine walioko madarakani na vilevile kwa korti hiyo yenyewe. Ikiwa ICC itaamuwa kuwa uamuzi wa Afrika Kusini kumuachia Bashir kuondoka kilikuwe kitendo cha ukiukaji, korti hiyo inaweza kuishitaki serikali ya Pretoria mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa au kwa wanachama wa ICC. Katika matukio yote, Afrika Kusini inaweza kupata  pigo la kidiplomasia kwa kukaripiwa na Korti hiyo, na siyo kutozwa faini yoyote au kuwekewa vikwazo. Kuna uwezekano pia kwa mahakama hiyo kukubaliana na hoja ya Afrika Kusini kwamba haikuwa na wajibu wa kutekeleza waranti wa kukamatwa kwa Bashir. Afrika Kusini inahoji kwamba waranti wa ICC wa kukamatwa Bashir ulikuwa batili mbele ya sheria zake zinazotoa kinga kwa marais walioko madarakani dhidi ya kushitakiwa, kufuatana na sheria ya kimataifa. Hata hivyo sheria za ICC zinabainisha wazi kwamba marais walioko madarakani hawana kinga katika kesi za uhalifu wa kivita.