1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubalozi wa Israel nchini Mauritania washambuliwa na watu wasiojulikana

1 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D15m

NOUAKCHOUTT:

Watu wenye bunduki ambao hawajatambulika,wameushambulia ubalozi wa Israel katika mji mkuu wa Mauritania-Nouakchoutt,ambapo wamewajeruhi watu kadhaa.Polisi inasema baa moja karibu na mahali hapo pia ilishambuliwa wakati washambuliaji walipokuwa wanatoroka kutoka mahali pa shambulio mapema leo asubuhi.Shambulio hilo limekuja wiki chache baada ya mashindano ya mbio za magari ya Lisbon –Dakar kuahirishwa kutokana na hofu ya tisho la wapiganaji wakiislamu katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.Mwezi Disemba,watalii wanne ,raia wa Ufaransa,pamoja na baadhi ya wanajeshi waliuawa katika matukio mawili tofauti.