1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANC yathibiti kuwa na nguvu kubwa

Abdu Said Mtullya23 Aprili 2009

Chama tawala ANC kinaongoza kwa asilimia karibu 60 wakati chama kipya cha upinzani COPE kimefikia asilimia 8.7 tu.

https://p.dw.com/p/HcLS
Washabiki wa chama cha ANC mjini PretoriaPicha: picture-alliance/ dpa

PRETORIA.

Hesabu za awali katika uchaguzi mkuu nchini Afrika Kusini zinaonesha kuwa chama  kinachotawala ANC kipo mbele sana, wakati chama kipya cha upinzani Congress of the People kimeshindwa kupiga hatua kubwa. Kura karibu alfu  23 zimeshahesabiwa kati ya idadi ya milioni 23  zinazotarajiwa.

Chama cha ANC kinaongoza kwa asilimia karibu 60 wakati chama kipya cha upinzani  kimefikia asilimia 8 nukta 7 tu.

Na chama kikuu cha upinzani ,Democratic  Alliance kipo katika asilimia 26.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba chama kipya cha Cope kilichotarajiwa kuwa changamoto kubwa kwa chama kinachotawala   hadi sasa kimeshindwa kukatua sehemu kubwa.