1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Angola

5 Septemba 2008

Uchaguzi umeanza nchini Angola kulichagua Bunge la viti 320.

https://p.dw.com/p/FBwP
Jose Eduardo dos Santos.Picha: picture-alliance/ dpa

Waangaola milioni 8.5 wanapiga kura hii leo ikiwa mara ya pili tangu uchaguzi wa 1992 kulichagua Bunge jipya.Ni nia ya serikali kuwa uchaguzi huu uwe wazi na bila ya mizengwe na uwe tofauti kabisa na ule wa Kenya na Zimbabwe.Lakini, wachunguzi wengi wasioegemea upande wowote wana shaka shaka kwamba itakuwa hivyo.

Tayari Upinzani unadai chama tawala cha MPLA kimeanza vitisho dhidi ya wapinzani. Nguvu za chama-tawala cha MPLA -ambacho tangu uhuru kutoka Ureno miaka 33 iliopita kinatawala mfululizo ,ni kubwa mno ukilinganisha na upinzani.Isitoshe, Rais Jose Eduardo Dos Santos na chama chake hawako tayari kugawana madaraka tangu na upinzani hata na jumuiya za kiraia.Si ajabu kwahivyo, kampeni ya uchaguzi wa leo iliendeshwa kwa nguvu zisizolingana baina ya serikali na upinzani.

Rais Eduardo dos santos anasema:

"Tunataka jambo moja tu:Kura za waangola kupigiwa chama cha MPLA.iishi MPLA-kutoka Cabinda hadi Cunene-ni taifa moja.Vita vinaendelea na ushindi hakika ni wetu."

Katika kitongoji cha mji mkuu Luanda kiliopo chini ya hali ya hatari, "Pai Grande" mzee mkongwe-rais Dos Santos amefika binafsi kuhudhuria mkutano wa mwisho wa kampeni ya uchaguzi ya chama-tawala cha MPLA.

"Mkongwe" kama wafuasi wake wanavyomuita "Pai Grande" haruhusu mambo kutokea kwa sadfa tu.La hasa.Kwani, amedhibiti madaraka kitambo kirefu mno na anaelewa hila zote.Zaidi ya miaka 30 amengangania hatamu za uongozi.

Hofu kwake ni kubwa mno kwake kuja kupoteza madaraka ili asije kushtakiwa kwa tuhuma za mapendeleo ,rushua na ufisadi.

Polisi wa kikosi maalumu wameweka njia safi ya kuelekea Kikolo.Afisi zote za serikali na hata maduka yamefungwa.Mabasi 10.000 na taxi ziliwasafirisha wafuasi wa chama-tawala mkutanoni.Gharama zote kimebeba chama tawala cha MPLA.Kila wendapo kumetapaa kofia za alama ya chama,bendera na T-shirt zikiwa na picha ya rais .Kwani rais Dos Santos haachi mambo kutokea bila mpango.

Uchaguzi wa leo lakini hauhusu kuchaguliwa rais bali bunge la viti 320 ambalo madaraka yake ni madogo tu.Vyama 10 mbali mbali na 4 vilivyounda Ushirika vinashiriki katika uchaguzi huu wa leo.Uchaguzi wa rais utafanyika mwakani.

Mfuasi mmoja wa chama-tawala cha MPLA hana shaka kuwa chama chake kitashinda kwa kishindo:

"Leo ni siku ya furaha kubwa kwa sababu tumepata fursa ya kuonana na Kiongozi wa chama chetu cha MPLA.Tumekuja hapa ili kuwa karibu na babu yetu Jose Eduardo dos Santos na kumpa nguvu.Tunajua kwamba chama chetu kimeshashinda,kwani ushindi hauwezi tena kupokonywa MPLA.Licha ya kujua hayo tumekuja kwa wingi hapa."

Chama kikubwa cha upinzani katika uchaguzi wa leo ni kile kilichokua cha waasi -UNITA.1992 UNITA iliafikiana mapatano ya kuweka silaha chini na serikali.B aada ya uchaguzi lakini vita vya kienyeji vikaripuka upya.Ni baada ya kuuwawa kwa kiongozi wake Jonas savimbi hapo 2002 ndipo amani iliporejea Angola.

Mada kuu ya chama cha UNITA ni rushua kubwa iliozagaa na mwanya mkubwa uliopo kati ya masikini wengi na matajiri wachache.thuluthi-mbili ya waangola wanaendelea bado kushi kwa pato lisilo zidi dala 2 kwa siku.Umri wa kushi wa wastani ni miaka 40.Tofauti za kimaisha mjini Luanda, mji mkuu ni kubwa mno.

Upande mmoja ufukara mkubwa na upande mwewngine ,katika mtaa wa ilha, mabwanyenye wanakunywa wiski na champainge watakavyo.isitoshe katika barabara za Luanda, magari ya kifahari yanapita na kusababisha msongamano zaidi kuliko katika jiji lolote kuu la Afrika. Ni chini ya hali hii,waangola milioni 8.5 wanapiga kura leo.