1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Burundi wawadia

Admin.WagnerD20 Julai 2015

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, anaonekana kujiandaa kushinda awamu ya tatu mfululizo ya uchaguzi tata wa urais uliopangwa kufanyika kesho, ushindi ambao utamfanya aliongoze taifa lililogawanyika kwa vurugu

https://p.dw.com/p/1G1VO
Burundi Parlamentswahlen
Uchaguzi Bunge la BurundiPicha: picture-alliance/dpa/D. Kurokawa

Tayari, upinzani na vyama vya kiraia vimeupinga ushiriki wake katika kinyang'anyiro hicho kwa kusema unakwenda kinyume na katiba ya Burundi na vile vile kinyume na mkataba wa amani, ambao ulifikisha kikomo miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na mauwaji ya halaiki ya kikabila ya mwaka 2006.

Kwa uchaguzi huo ambao upinzani umelalamika ni mchakato batili, Pierre Nkurunziza, rais mwenye umri wa mika 51, muasi wa zamani, mkristo aliyezaliwa upya au Mlokole na mshabiki wa soka, hana mpinzani.

Sauti za upinzani

Leonce Ngendakumana, mmoja kati ya watu mashuhuli kwa upande wa upinzani nchini Burundi, akizungumza baada ya kuvunjika kwa mazungumzo yaliyokuwa yakiratibiwa na Uganda hapo jana alisema, "Serikali imeamua kujitenga na kuendelea na uchaguzi batili."

Mpinzani mwingine Jean Minani alisema "Ni hali ya kutowajibika kwa kiasi kikubwa, wamekaidi kuisaidia Burundi kutumbukia katika dimbwi".

Akizungumza maandalizi ya zoezi hilo la kesho mjini Bujumbura raia mmoja wa Burundi alisema "Ntashiriki zoezi la kupiga kura kama nilivyokuwa nikifanya siku zote. Tunampigia kura kiongozi tunaempenda, na ambae tufahamua ametufanyia mengi"

Zaidi ya miezi miwili iliyopita maandamano yalikuwa yakimpinga Nkurunziza yamesababisha vifo vya takribani watu 100, yaliotokana na ukandamizaji serikali.

Hali si shwari

Hali haikuishia hapo, vyombo vya habari vya kibinafsi vimefungwa na wapinzani wengi wamelikimbia taifa hilo na kujiunga na Warundi wengine wengi wa kawaida zaidi ya 150,000, ambao wameondoka nchini humo kwa kuhofia, pengine kwa mara nyingine tena taifa hilo linaweza kutumbukia katika machafuko makubwa.

Burundi Pressefreiheit
Waandishi wa habari wakipigania haki yaoPicha: Esdras Ndikumana/AFP/Getty Images

Katikati ya Mei, Majenerali waasi walijaribu kumpindua Nkurunziza, ingawa walishindwa. Taifa hilo dogo lisilo na bandari na moja kati ya mataifa masikini kabisa barani Afrika, limekuwa kitovu cha machafuko katika eneo la Kanda ya Maziwa Makuu.

Wachambuzi wanasema kuibuka upya kwa machafuko katika taifa hilo, kunaweza kuchochea upya vurugu kati ya Wahutu na Watutsi na kuzusha janga kubwa la kibinaadamu katika eneo hilo, ambalo linaweza kusababisha hatari pia katika mataifa jirani zaidi ya inayosababishwa na ile inayotokana na vita vya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ikumbukwe vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Burundi vilisababisha vifo vya watu 300,000.

Kundi la vijana kutoka chama tawala cha CNNDD-FDD. Imbonerakure, ambalo limepewa hadhi ya wanamgambo na Umoja wa Mataifa na limekuwa likirejesha kumbukumbu za zama za Wahutu wenye misimamo mikali ambao waliongoza mauwaji ya Kimbari ya Rwanda.

Kwa lengo la kutuliza kitisho cha amani ya Burundi, Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Afrika Mashari yenye kuundwa na matifa matano, imekuwa ikifanya jitihada za upatanishi pasipo mafanikio. Hapo jana Jumapili chanzo kimojan kutoka EAC kilisema jitihada za mwisho za upatanishi zilitzokuwa zikiongozwa na Waziri wa Ulinzi wa Uganda Crispus Kiyonga, kwa hivi sasa zinaonekana zimekufa.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP
Mhriri:Josephat Charo