1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika Oktoba, 28

Sudi Mnette
21 Julai 2020

Tume ya Uchaguzi ya Tanzania imesema watanzania watamchagua rais wa nchi hiyo, pamoja na wabunge na madiwani katika uchaguzi mkuu hapo Oktoba 28.

https://p.dw.com/p/3fdlU
Afrika Tansania Präsidentschaftswahlen 2020
Picha: DW/S. Khamis

Ibara ya 41 kifungu cha nne cha katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania 1977 pamoja na marekebisho yake, ikiambatana na vifungu kadhaa katika sheria ya uchaguzi pamoja na sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa sura ya 292, inatoa kibali kwa tume hiyo kutangaza ratiba ya uchaguzi.

Akitumia takriban dakika mbili kuutangazia umma ratiba ya uchaguzi mwenyekiti wa NEC jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa Semistokles Kaijage amesema, mbali na mambo mengine kampeni za uchaguzi zitaanza rasmi Agast 26 hadi Oktoba 27 mwaka huu, huku tarehe ya uchaguzi ikianguakia siku ya jumatano ambayo ni Oktoba 28.

Tume ya uchaguzi yatoa maelezo bila ya kuruhusu maswali

Präsident John Magufuli aus Tansania
Rais John Magufuli wa TanzaniaPicha: Getty Images/AFP/M. Spatari

Aidha tume hiyo haikutaka kuruhusu maswali kupeleka uchaguzi kuwa siku ambayo itakuwa ni katikati ya juma, licha ya wanahabari kujiandaa na maswali ya kuhoji zaidi. Itakumbukwa kuwa chaguzi zilizopita tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi takriban miongo miwili sasa, tanzania ilizoeeleka uchaguzi kufanyika jumapili ya mwisho wa mwezi wa kumi, hatua ilioleta mazoea miongoni mwa wananchi kuwa huenda hata uchaguzi wa mwaka huu ungelifanyika katika tarehe hizo.

Rais John Magufuli  wa taifa hilo atawania  muhula  wa  pili , baada  ya  kuteuliwa  kuwa  mgombea  wa  chama  tawala  mapema  mwezi huu. Magufuli  ambaye  alichaguliwa  kuwa  rais mwaka  2015, katika  muhula  wake   wa  kwanza  alishutumiwa  kubana  uhuru wa kujieleza, akizidisha uongozi wa  mkono wa chuma na kuzuwia taarifa za  janga  la  virusi  vya  corona  nchini humo. 

Soma zaidi: Membe kuwania urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo.

Nchi hiyo  haijatoa taarifa  rasmi  za  kesi  za  maambukizi  ya  virusi  vya  corona  tangu Aprili 29,  tofauti na  nchi  jirani  haijachukua  hatua  zozote kupambana  na  virusi. Jana, Magufuli alisisitiza  madai  yake  kuwa  Tanzania  haina tena wagonjwa  wa  COVID - 19, na kuwataka  watalii  wa  kimataifa  kutembelea nchi hiyo.