1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Tanzania

31 Oktoba 2010

Watanzania wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa urais.

https://p.dw.com/p/Pul9
Rais Jakaya Kikwete.Picha: DW

Watanzania wanapiga kura hii leo  katika uchaguzi wa urais ambao huenda ukampa uongozi kwa mara ya pili na ya mwisho , rais aliyepo  madarakani Jakaya Kikwete katika nchi hiyo iliyo ya pili kwa ukubwa kiuchumi,Afrika mashariki.

Rais Kikwete alichaguliwa kwa wingi wa asilimia 80.2 ya kura mnamo mwaka 2005 na  wakati  maoni ya  awali  ya wapiga  kura  yalimpa  nafasi  kubwa  ya uongozi ,  hali  hiyo  imepadilika  katika  wiki  za  mwisho  za  kampeni   na baadhi  ya wachambuzi wanadai  kuwa  idadi kubwa ya wananchi wanaoatarajiwa  kujitokeza  kupiga  kura huenda wakapiga kura  zao  kwa upinzani.Tanzania ni nchi iliyo imara katika eneo ambalo kwa mara nyengine hukosa utulivu na imefanikiwa kufanya chaguzi  za vyama vingi vya kisiasa mara tatu tangu mwaka 1995, baada  ya utawala wa zaidi ya miongo mitatu wa chama kimoja.

Beobachter in Tansania
Waangalizi wa uchaguzi mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Ulaya.Picha: EUEOM

Mpinzani mkuu wa rais Kikwete katika uchaguzi huu, Wilbrod Slaa wa chama cha CHADEMA, ametoa wito kwa wapiga kura kumpa nafasi ya kupambana na rushwa na kuendeleza huduma kama vile za afya na elimu katika nchi hiyo iliyo maskini.

Mwandishi Maryam Abdalla/RTRE.

Mhariri:Sekione Kitojo.