1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Thailand

23 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CfQI

BANGKOK:

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Thailand yaonesha ushindi kwa vyama vilivyoshirika na waziri mkuu wa zamani aliepinduliwa madarakani Thaksin Shinawatra.Wachunguzi waona matokeo haya yamkini yakachimba zaidi kaburi la mzozo wa kisiasa wa miaka 2 sasa nchini Thailand.

Matokeo ya uchunguzi kutoka vituo 2 tofauti vya Thailand yatafautiana juu ya ukubwa wa ushindi huo iwapo kikundi kinachoelemea waziri mkuu wa zamani -Peoples’ Power Party, kitajipatia wingi mkubwa kuweza kutawala pekee katika Bunge la viti 480.