1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hillary Clinton arejea katika kinyang'nyiro chha uteuzi

Mtullya, Abdu Said5 Machi 2008

Baada ya kushindwa mara 11 mfululizo Seneta wa jimbo la New York Hillary Clinton amerejea tena katika kinyang'anyiro cha kuwania tikeki ya kugombea urais wa Marekani.

https://p.dw.com/p/DIK6
Seneta Hillary Clinton wa jimbo la New York.Picha: AP



Seneta  wa  jimbo la New York Hillary Clinton amerejea tena katika kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya chama cha Demokratik ya kugombea urais wa Marekani baada ya kushinda katika majimbo muhimu ya Texas na Ohio.

Lakini mpinzani  wake seneta  Obama bado anaongoza katika idadi ya wajumbe.


Baada ya kushindwa mara 12 mfululizo katika teuzi za kumtafuta mjumbe wa kukiwakilisha chama  cha demokratik katika kugombea urais waMarekani,seneta wa jimbo la New York   Hillary Clinton ameshinda  katika majimbo muhimu ya Texas na Ohio. Clinton pia ameshinda katika Rhode Island.


Seneta huyo amesema "mnajua msemo, inapoelekea Ohio ndiko linapoelekea taifa".

Hillary Clinton sasa yumo tena katika kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya kugombea urais.

Hatahivyo pamoja na ushindi katika majimbo hayo seneta Clinton hajafikia idadi ya wajaumbe alinayo mpinzani wake seneta Obama wa jimbo la Illinois.

Obama amesema bado anaongoza kwa idadi ile ile ya wajumbe kama hapo awali.  

Kinyang'anyiro cha kugombea uwakilishi huo bado kinaendelea katika chama cha Demokratiki.Yumkini si Obama wala Clinton atakaeweza kupata idadi ya wajumbe 2025 inayohitajika. Wajumbe wa ngazi ya juu 800 wanapaswa kuamua Wajumbe hao hawapo upande  wowote. Kindumbwe ndubwe hicho kitafanyika tena  tarehe 22 mwezi aprili.

Lakini katika chama cha Republican mshindi ameshapatikana.

Seneta John McCain wa jimbo la Arizona

ndiye atakaekiwakilisha chama cha Republican katika kugombea urais wa Marekani.