1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa baraza la jiji la Cologne bila ya mtetezi wake

Oumilkher Hamidou29 Machi 2009

Meya wa jiji la Cologne asema hataki ajali ya jumba la nyaraka ichanganywe na kampeni za uchaguzi

https://p.dw.com/p/HMHB

Cologne:

Meya wa jiji la Cologne,Fritz Schramma anasema hatogombwa tena wadhifa huo.Kwa kufanya hivyo,mwanasiasa huyo wa kutoka chama cha CDU,anajibebesha dhamana ya kuporomoka jengo la nyaraka za historia na majengo mengine kadhaa ya karibu na hapo.Fritz Schramma amesema hatotetea wadhifa huo uchaguzi utakapoitishwa Agosti 30 mwaka huu,ili kuuutenga msiba huo na kampeni za uchaguzi.Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 61 amekua akikosolewa tangu jengo la nyaraka za historia nkuporomoka March tatu iliyopita na kugharimu maisha ya vijana wawili.