1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Kosovo

12 Desemba 2010

Huu ndio uchaguzi wa kwanza Kosovo, tangu ijitangazie uhuru miaka miwili iliopita.

https://p.dw.com/p/QWFL
Uchaguzi wa kwanza Kosovo.Picha: AP

Wapiga kura  nchini  Kosovo leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza, tangu Kosovo kujitangazia uhuru wake kutoka Serbia mwaka  2008. Wagombea wakuu katika uchaguzi huo ni Waziri Mkuu Hashim Shah-Chi na mshirika wake wa zamani  katika  serikali  ya  mseto Isa Mustafa ambaye ni meya wa mji mkuu Pristina. Mustafa anatumia ngao ya vita dhidi ya rushwa katika kampeini yake, kwa lengo la kujipatia kura kutokana na hali mbaya ya uchumi ambayo imewavunja moyo wananchi wengi wa Kosovo. Katika uchunguzi mpya wa  maoni  uliotolewa  unaonyesha  kuwa asilia mia 73 ya raia wa Kosovo wanadhani kuwa rushwa imekuwa mbaya zaidi chini ya utawala wa Sha-Chi ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu ijitangazie uhuru wake. Tangu kujitangaza taifa huru Kosovo imetambuliwa na mataifa 72, ikiwemo Marekani na nchi 22 za Umoja wa Ulaya ispokuwa tano za Umoja huo wenye wanachama 27. Umoja wa Ulaya umeitaka Kosovo kuhakikisha kuwa uchaguzi wake huo wa kwanza  unakuwa  huru na wa haki.