1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa rais Russia

28 Februari 2008

Warusi wanapiga kura jumapili hii kumchagua rais anejulikana kabisa:Dmtry Medvedev.

https://p.dw.com/p/DFNF
Dmitry Medvedev (kulia)Picha: AP

Warusi wanapiga kura jumapili hii ijayo kumchagua rais mpya ambae hakuna shaka atakuwa Dimitry Medvedev,mtu ambae rais anaeacha wadhifa huo Vladmir Putin, amemfungulia njia hiyo.

Ingawa uchumi wa Russia unastawi ,wanauchumi wanaonya rais huyo mpya ajae atakabiliwa na changamoto kubwa ikiwa anataka kuselezea kustawi huko kwa uchumi nchini Russia.

Ramadhan Ali anatufungulia pazia kabla uchaguzi wa rais wa jumapili hii:

Maafisa wa utawala na wanabiashara madukani wamekuwa wakinin’niza picha za Dmitry Medvedev na hata mashuleni wakifuata mtindo ulianzia zama za Tsar na dola la kisoshalist la Urusi.

Tangu ilipotangazwa kuwa Medvedev ndie atakerithi kiti cha Wladmir Putin kama rais wa Russia ,haikukawia kupokea maombi ya picha zake na zimekuwa zikiuza hata zaidi kupita zile za rais Putin-alisema mwenye duka la picha mjini Moscow.

Uchaguzi ukinyemelea jumapili hii ,kiasi cha 70% cha wananchi wanataka picha za

Baada ya kuchaguliwa Medvedev rais mpya wa Russia jumapili hii, rais wa zamani Wladmir Puti atahamia wadhifa wa waziri mkuu chini ya mtu aliempendekeza Medvedev.

Hadi sasa Dmitry Medvedev akishika wadhifa wa makamo wa kwanza wa waziri-mkuu.

Russia ikikaribia kupata rais mpya inapigana wakati huu kudhibiti kufurika kwa bei.Mwaka jana ughali wa maisha ulifikia kima cha 11.9% kinyume na shabaha ya serikali ya kukiweka kiwango hicho 8%.Kutimiza shabaha hiyo, serikali ya Putin iliruhusu sarafu ya Rouble kupanda thamani –hatua ambayo haikufanya kazi kushusha ughali wa maisha.Hatua hiyo pia ilidhuru viwanda vya ndani vya Russia kwavile ilifanya bidhaa zao kuwa ghali nchi za nje.Kwahivyo, mjadala motomoto juu ya jinsi gani kupambana na ughali wa maisha uko usoni nchini Russia.

Bajeti ya Russia inategemea mavuno ya fedha za mafuta na gesi yake inayouzwa nchi za nje.Na hali hii inaifanya Russia kuweza kujeruhiwa bei za nishati hizo zikianguka masokoni kutokana na msukosuko wa uchumi ulimwenguni.

Serikali ya Russia imetangaza mpango wa kufidia bei za umeme na gesi kwa matumizi ya nyumbani,lakini umekuwa ukienda pole pole kuutekeleza.Bei za ndani za nishati kwa jumla ziko chini lakini shabaha ni kuziachia bei za gesi na petrli kufikia viwango vya dunia ifikapo 2011.Nyongeza hizo huenda zisiwapendeze wapigakura jumapili hii.

Wakaazi wa Russia wanakonga.Na ikiwa malipo ya uzeeni hayatafanyiwa mageuzi ,hakutakua na walipakodi wakutosha kugharimia michango yao katika mfuko wa bima ya uzeeni miaka michache ijayo.Tayari kuna kasoro katika mfuko huo.Na serikali haina sera wazi ya kupüambana na ukosefu huo.Suluhisho moja lililopendekezwa la kuwahimiza warusi kuweka akiba kwa siku zijazo badala ya kuitegemea serikali,huenda lisiwapendeze wananchi .

Akichaguliwa rais jumapili hii nah ii haina shaka, Dmitry Medvedev yamkini atabakia na timu ile ile atakayorothi kutoka kwa Bw.Putin,ingawa wachunguzi wa mambo yapitayo Kremlin,watazamia mageuzi madogo ya baraza la mawaziri.