1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa rais wafanyika leo Serbia

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1dV

Uchaguzi wa rais unafanyika leo nchini Serbia. Waserbia wanachagua kati ya rais Boris Tadic na mpinzani wake Tomislav Nikolic, ambao wanakabana koo katika kinyang´anyiro kitakachoamua mkondo utakaochukuliwa na Serbia kuhusu Umoja wa Ulaya.

Rais Tadic anachukuliwa kuwa kiongozi anayeegemea zaidi nchi za magharibi na anataka kuilekeza Serbia katika Umoja wa Ulaya.

Mpinzani wake Nikolic kwa upande wake anataka kulielekeza taifa hilo la Balkan upande wa Urusi.

Mojawapo ya maswala muhimu katika uchaguzi wa leo ni hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo.

Nchi nyingi za Umoja wa Ulaya zinataka jimbo hilo liwe huru kutoka kwa Serbia, lakini serikali ya mjini Belgrade inapinga hatua hiyo.