1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa urais nchini Rwanda mwaka 2010

26 Oktoba 2009

Ntaganda Bernard Abdulkarim athibitisha kuwania kiti cha urais kwa chama cha PS Imberakuri

https://p.dw.com/p/KFlZ
Jiji la Kigali,RwandaPicha: James Nzibavuga

Uchaguzi wa urais nchini Rwanda umepangwa kufanyika Agosti mwaka ujao wa 2010, ambapo chama cha PS Imberakuri kimemteua Ntaganda Bernard Abdulkarim kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho. Bwana Ntaganda, ndiye mgombea wa kwanza kuthibitisha atawania kiti hicho katika uchaguzi ujao, huku akiwa amekuja na mtindo mpya wa kuongelea kwa uwazi baadhi ya mambo nyeti katika siasa za sasa nchini humo, kitu ambacho wanasiasa wengi wamekuwa wakijaribu kukiepuka kwa hali zote. Mwandishi wetu mjini Kigali, Daniel Gakuba, amezungumza naye na alianza kwa kuelezea historia yake.

Mahojiano: Daniel Gakuba/Ntaganda Bernard

Mpitiaji: Grace Patricia Kabogo