1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wafanyika leo Pakistan

Abdu Mtulya18 Februari 2008

Rais Musharraf asema atashirikiana na serikali mpya itakayoundwa bila kujali chama kitakaoshinda uchaguzi

https://p.dw.com/p/D9Br
Wanaume wa Pakistan wakionyesha vitambulisho vyao kabla kupiga kura huko Hyderabad hii leoPicha: picture-alliance/ dpa

Watu wa Pakistan leo wanapiga kura kulichagua bunge jipya linaloweza kuashiria mwisho wa utawala wa rais Pervez Musharraf.

Kwa mujibu wa kura za maoni, chama cha Pakistan People's Party cha hayati Benizir Bhutto kinatarijiwa kushinda .

Uchaguzi wa leo nchini Pakistan unafanyika huku kukiwa na hofu kubwa ya mashambulio ya kuuvuruga. Watu 47 waliuawa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa hadhara kutokana na shambulio la kigaidi. Na wakati huo huo vyama vya upinzani pia vinadai kwamba vyama vinavyofungamana na rais Musharraf vinakula njama za kuiba kura.

Watu wapatao milioni 80 waliotolewa mwito wa kupiga kura ili kulichagua bunge jipya walianza kumininika kwenye vituo vya kupigia kura mapema asubuhi leo.

Lakini msemaji wa chama cha upinzani cha PPP amedai kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru na wala hautakuwa wa haki kutokana na njama za chama kinachomuunga mkono rais Musharraf za kutaka kufanya udanganyifu wa kura.

Kiongoziwa chama cha upinzani cha Musli League , aliekuwa waziri mkuu waPakistan bwana Nawaz Sharrif pia ameta madai juu ya kufanyika njama .Amedai kuwa watu wanaomwuunga mkono rais Musharraf wana mpango kabambe wa kuiba kura.

Uchaguzi wa leo nchini Pakistan pia unafanyika huku kukiwa na hofu kubwa ya kutokea mashambulio ya kigaidi.Hayo yanatokana na kutambua kwamba watu 450 wameshaua mnamo mwaka huu kutokana na mashambulio ya kigaidi nchini Pakistan.Wasi wasi huo unawaeza kusababisha watu wachache tu wajitokeze kupiga kura, jambo litakalokuwa na manufaa kwa wanaofungamana na rais Musharraf.

Serikali ya bwama Musharraf imetoa wanajeshi alfu 80 watakaoshirikiana na polisi katika kulinda amani.

Licha ya matumaini ya kushinda katika uchaguzi wa leo pana wasi wasi juu ya mustakabal wa chama cha hayati Bhutto PPP. Juu ya wasi wasi huo mwandishi habari maarfu wa Pakistan Ashraf Khan ameeleza.

Kwa sasa chama hicho kipo pamajo kutokana na kampeni ya uchaguzi inayoenda vizuri. Suala muhimu kwa chama hicho linahusu uongozi:kwa sasa Zardari-mume wa hayati Bhutto- anaongoza chama hicho lakini katika siku za usoni mgogoro mkubwa utatokea.

Lakini mjumbe wa chama hicho amesema chama chao hakina mgooro wa uongozi na katika uchaguzi wa leo anatarajia ushindi mkubwa wa chama chake.

Uchaguzi huo mkuu ulikuwa ufanyike tarehe nane mwezi januari lakini uliahirishwa kutokana na kifo cha Bhutto alieuliwa katika shambulio la kigaidi.

Matokeo yanatarajiwa kuanza kufahamika usiku wa leo. Wataalamu wanatabiri kuwa hakuna chama kitakachopata wingi mkubwa katika bunge lenye viti 342. La kutilia maanani ni nani ataunda mseto na chama cha PPP.

Wasiwasi juu ya wizi wa kura unaweza kusababisha vyama vya upinzani vikatae matokeo ya uchaguzi huo.