1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi na mazingira

10 Mei 2012

Katika mfululizo wa vipindi vyetu kuhusu masuala ya uchumi na biashara, na pia kuhusu mazingira, unapata taswira kamili jinsi maisha ya kawaida kila siku yanavyoathiri au kuathiriwa na sehemu nyingine za ulimwengu.

https://p.dw.com/p/LOXP
Picha: LAI F

Noa Bongo inakupa fursa wewe msikilizaji kufahamu vyema matatizo na maajabu ya Ulimwengu- yaani hali ilivyo kwa jumla katika karne hii ya 21. Katika mfululizo wa vipindi vyetu kuhusu masuala ya uchumi na biashara, na pia kuhusu mazingira, unapata taswira kamili jinsi maisha ya kawaida kila siku yanavyoathiri au kuathiriwa na sehemu nyingine za ulimwengu. Mfano katika mchezo wa redio kuhusu masuala ya uchumi tunaona jinsi uchumi na biashara unavyoendeshwa katika soko la ndani na la kimataifa kupitia vijana wawili walioanzisha biashara yao ndogo na hatimaye kupanuka na kuwa watu mashuhuri katika uchumi wa kimataifa.

Fursa za Ulimwengu na changamoto za kimataifa

Na ili kufahamu vyema jinsi uchumi wa kimataifa unavyoendeshwa, vipindi vya Noa Bongo vinaeleza utaratibu mzima wa utandawazi wa kiuchumi na jinsi unavyoathiri shughuli za vijana barani Afrika. Kujiingiza katika uchumi wa ulimwengu kunamaanisha kuyavulia nguo matatizo ya ulimwengu.

Na katika mfululizo wa vipindi vyetu kuhusu mazingira, wanafunzi wanne wanahoji kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na kufahamu athari zinazosababishwa na hali hii.

Lakini, iwe ni kwa manufaa ya kiuchumi au matatizo ya kimazingira, vipindi vya Noa Bongo vinakupa wewe msikilizaji muongozo na jinsi unavyoweza kuyashughulikia masuala haya, kila siku mahali popote ulipo.