1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Udondozi wa Magazeti unagusia zaidi hali ya kisiasa Hamburg

Saumu Ramadhani Yusuf29 Novemba 2010

<p>Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo hii wamejishughulisha zaidi na matokeo ya kisiasa huko Hamburg, yaani kuvunjika kwa serikali ya mseto ya CDU na Kijani

https://p.dw.com/p/QKvp
Serikali ya mseto wa CDU na kijani HamburgPicha: dapd

Tuanze na Gazeti la  Kieler Nachrichten linalozungumzia sintofahamu ya kisiasa huko Hamburg:

Muhariri wa Gazeti hilo anasema hadi sasa mafanikio ya chama cha Kijani ni hisia tu. Chama hicho sasa kimekuwa kama kipofu na kwa hivyo basi kimefikia hatua ya hadi kuamini kwamba kinaweza kusimama peke yake. Gumzo lililoko sasa ni juu ya muungano  wa chama cha SPD na Kijani, ingawa pia mradi huo umeshawahi kuwepo na kufa siku za nyuma. Na hii ndio sababu, bila shaka, chama cha Kijani kinapendelea tena muungano wa chama chake na SPD. Hata hivyo, kwa hali ya upepo wa kisiasa unavyovuma huu unaonekana kama ni mchezo wa pata potea.Kwa hivi sasa umaarufu wa chama cha kijani haukifaidii kwa vyocvyote chama cha SPD. Na ni nani aliyesema kwamba hata chama cha SPD kikishindwa uchaguzi ukifanyika kitakuwa tayari kuwa mshirika mdogo katika serikali ya muungano wa chama chake na Kijani? Kitisho hicho hakiwezi kupata nafasi Hamburg, lakini huko BadenWuttemberg kinawezekana.

Muhariri wa gazeti la Sächsiche Zeitung yeye anasema:

Mwisho wa safari ya chama cha CDU na Kijani huko Hamburg unakwenda sambamba na mkakati wa Kansela Angela Merkel. Kwa muda wa wiki kadhaa zilizopita,  Kansela amekuwa akikitetea chama chake kutokana na uchaguzi ujao katika jimbo la Baden Wurttemberg dhidi ya  chama cha Mazingira. Na endapo chama cha CDU kitapoteza nafasi ya uongozi huko Stuttgart, bado Kansela atakuwa katika kitisho.Kwa mantiki hiyo, muungano wa FDP na CDU  dhidi ya SPD na Kijani ni mpambano unaoweza kushuhudiwa. Hata hivyo, bado hapajatolewa neno la mwisho kuhusu suala la muungano wa CDU na Kijani. Wapiga kura wengi wanatia hesabu vingine na vile wenye kufanya mikakati katika makao makuu ya vyama vya siasa wanavofikiria

Gazeti la Nördwest Zeitung pia linazungumzia kuhusu hali ya kisiasa huko Hamburg. Muhariri wa Gazeti hilo, yeye anahisi:

Wasiokuwa pamoja  hapo kitambo hawawezi kushirikiana. Muungano wa CDU na Kijani Hamburg umevunjika katika hali ya kustaajabisha kama muungano huo ulivyoanzishwa. Pakitokea hivi sasa manunguniko kutika Chama cha CDU kwamba kimeshangazwa na kuvunjika ndoa hiyo, basi huo ni tu nusu ya ukweli .Nani na vipi Kansela na washirika wake walioko madarakani wanaosema kwamba kuundwa kwa serekali ya mseto baina ya chjama  hicho na cha Kijani katika ngazi ya shirikisho ni uwandawazimu, basi wasistaajabu kwamba jambo kama hilo la muungano linaoonekana kuwa ni jambo ambalo ni changa bado.

Tukigeukia mada yningine Gazeti la Berliner Zeitung limeandika kuhusu kashfa ya Wiki Leaks:

Muhariri wa Gazeti hilo anasema

Mtandao wa Wiki Leaks umeweka bayana; mamia kwa maelfu ya taarifa za siri na kuzusha hali ya kutoaminiana.Taarifa hizo zinahusu kuanzia masuala ya watu binafsi hadi siasa na kuidhoofisha nafasi ya Marekani katika  jukwaa la Kimataifa na zaidi kuifanya hali kuwa ngumu linapohusika suala zima la diplomasia.

Kwa hali kama hiyo muhariri anasema

Utawala wa Marekani unabidi kujiuliza ni kwanini nchi kubwa kama hiyo inayopeleka watu hadi mwezini na kudengua  maroketi angani inaweza kuanguka katika mtego kama huu, na taarifa zake za ndani kuweka bayana kwenye mtandao? Ni vipi afisa wake anaweza kukiuka sheria za ndani katika nchi yenye nguvu kama hiyo na kuzusha aibu kubwa kiasi hicho?

Ama upande wake muhariri wa hgazeti la Süddeutsche Zeitung mtazamo wake ni kwamba: 

Je ni sawa Mtandao wa Wiki leaks kutoa taarifa za siri za serikali hadharani. Iikiwa vyombo vya habari vinafanya hivyo, basi unaweza kuzichuja taarifa,kuzipanga na kulinda haki za watu. Ikiwa mtandao huo unaweza kuchapisha nyaraka nyingi kiasi hicho basi vipi  ni wazi kwamba mtandao huo haudhibitiwi wala kuchunguzwa. Na kwasababu mmliki wa mtandao huo ana uwezo wa kitechnologia basi ni wazi kwamba anaweza kuzionyesha  taarifa atakazo katika mtandao,kwa rafiki zake au hata kwa wafanyikazi wake. Kashfa kama hii inadhihirisha kwamba Diploamasia katika Wizara ya mambo ya Nje na Ndani sio siku zote inafanya kazi.

Mwandishi;  SaumU Yusuf

Mhariri: Miraji Othman