1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Udondozi wa maoni ya wahariri wa Ujerumani.

Sekione Kitojo27 Mei 2009

Wahariri wameandika kuhusu Korea ya kaskazini, upunguzaji wa deni la serikali pamoja na suala la kuuzwa kwa kampuni ya Opel.

https://p.dw.com/p/HyEw
Kiongozi wa Korea ya kaskazini Kim Jong Il .Picha: AP Graphics


Wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo wameandika kuhusu mada nyingi. Lakini wengi wamezungumzia kuhusu hatua ya Korea ya kaskazini kufanya majaribio ya kinuklia, serikali ya Ujerumani kuzuwia deni kubwa zaidi la serikali, pamoja na suala la kampuni la kutengeneza magari la Opel kufilisika ama kuuuzwa.


Tukianza na mada ya Korea ya kaskazini: Gazeti la Der Neue Tag kutoka Weiden linaandika:

Hata Urusi na China ambazo zimekuwa zikiiunga mkono serikali ya Korea ya kaskazini na kwa hiyo kutakiwa na Marekani kutumia ushawishi wao kulidhibiti taifa hilo, hivi sasa wanatambua ni vipi mshirika wao huyo asiyetabirika alivyo.

Wamejenga jeshi lenye wanajeshi zaidi ya milioni moja, na sasa wana makombora, pamoja na utaalamu wa kutengeneza mabomu ya kinyuklia. Kim Jong Il anaelekeza kila kitu katika jeshi na kuwasukuma watu wa nchi hiyo katika matatizo ya njaa.

Gazeti la Lausitzer Rundschau kutoka Cottbus, kuhusiana na mada hiyo, linaandika:

Hadi sasa serikali ya China ndio iliyokuwa ikiusaidia utawala huu wa Korea ya kaskazini. Wanamuona kiongozi muovu wa nchi hiyo, Kim Jong Il, hana haja ya kuleta maendeleo ambayo yanaweza kuletwa kwa kuungana tena nchi mbili za Korea. Lakini hata mjini Beijing utawala wa nchi hiyo unatambua kuwa utawala wa Korea ya kaskazini ni kitisho, na hususan utawala huo hautabiriki kwa kuwa hauwezi kuleta maendeleo mengine.

Nalo gazeti la Fränkischer Tag , kutoka Bamberg linaandika:

Tatizo linaloikabili dunia nzima , wakati taifa hili lililotengwa linazidi kujitenga, ni vipi mtu anaweza kulishughulikia na taifa kama hili ambalo halijali? Tutafanya nini iwapo juhudi za kidiplomasia zinakwama? Ni vikwazo gani vya kiuchumi dhidi ya utawala wa nchi kama hii vinaweza kuwekwa, ambapo raia wenyewe wa nchi hiyo tayari wako kama mateka.?

Mada yetu ya pili inahusu serikali ya Ujerumani kupunguza deni lake la serikali: Gazeti la Rhein Zeitung kutoka Koblenz linaandika:

Mchezaji mpira awapo mita moja mbele ya goli lililowazi, kwa lugha ya soka, wanasema ni asilimia mia moja ya nafasi ya kufunga, nafasi kama hiyo asingeipata tena mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, Mario Gomez. Lakini nafasi kama hiyo ipo kwa serikali ya mseto mjini Berlin. Upunguzaji wa deni ambao unatokana na katiba na ambao utajadiliwa katika bunge siku ya Ijumaa, si wa mtu mmoja , bali uamuzi wa muda wa kufikiwa hatua hiyo kwa serikali yote.

Nalo gazeti la Heilbronner Stimme linaandika:

Rekodi ya nakisi katika mwaka huu ya Euro bilioni 48 imevunjwa, zimeongezwa bilioni tatu zaidi. Ni hatua ngapi ndogo zitachukuliwa pamoja na kufanya mabadiliko ya kodi ya mapato kwa wafanyabiashara wadogo ama hali bora zaidi ya masoko ya bima kama njia ya kutoa msaada wa kichocheo cha uchumi. Serikali inasema tutatekeleza hatua ya kupunguza deni , kuanzia mwaka 2020.

Mada yetu ya mwisho inahusu kampuni la Opel. Gazeti la Oldenburgische Volkszeitung linaandika:


Iwapo serikali ya Ujerumani kuhusiana na suala la kampuni ya Opel na kila nafasi iko wazi , basi ni hakika kuwa hakuna kosa kwa mada iliyotolewa na waziri wa uchumi, Karl-Theodor zu Guttenberg, kuhusu hali ya kufilisika kampuni hiyo kudurusiwe upya.



Mwandishi Sekione Kitojo/Agenturen


Mhariri Othman, Miraji