1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UEFA: Timu 24 hazijaathiri Euro 2016

21 Juni 2016

Ongezeko la timu hadi 24 katika kombe la Ulaya, Euro 2016 halijaathiri ubora wa mchezo licha ya kuwa michezo hii imeshuhudia magoli machache kuliko mashindano yaliyopita

https://p.dw.com/p/1JALh
Frankreich Fußball-EM Slowakei vs. England Fans
Picha: Reuters/J. Cairnduff

Hayo ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa mashindano wa UEFA Giorgio Marchetti. Marchetti amewaambia waandishi habari , kwamba "ameshangazwa kwa upande wa njia chanya " wakati timu nane zilizoongezwa na mfumo tata uliopo "haukuweza kuwa na athari hasi " katika mashindano hayo.

Marchetti amesema makundi bado yako wazi na kwamba UEFA pia haitarajii udanganyifu katika duru ya mwisho ya makundi kwasababu timu nyingi zinahitaji ushindi kuweza kupata nafasi ya kufika katika duru ya mtoano.

Kampuni inayotengeneza vifaa vya michezo ya Puma imesema leo inaangalia kuhusu sababu zilizosababisha jezi nne za timu ya taifa ya Uswisi kupasuka wakati wa michuano hii ya Euro 2016 hapo jana dhidi ya Ufaransa.

"Wataalamu wetu wa bidhaa wanachunguza nyuzi za jezi hizo. Tutatoa taarifa hivi karibuni wakati tutafahamu sababu ya kutatuka jezi hizo kirahisi," amesema msemaji wa kampuni hiyo katika mji wa kusini wa Ujerumani wa Herzogenaurach. Ameongeza kwamba tatizo hili halijawahi kutokea hapo kabla. Puma wanatengeneza jezi za timu ya taifa ya Uswisi pamoja na timu nyingine nn zinazoshiriki katika fainali hizo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / ape / afpe / dpae
Mhariri: Yusuf , Saumu