1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa kuanza kuondoa wanajeshi Mali mwezi Machi

6 Februari 2013

Majeshi ya Ufaransa yameua mamia ya wapiganaji wa Kiislamu katika mapigano ya kuirejesha sehemu ya kaskazini chini ya udhibiti wa serikali ya Mali, na sasa Ufaransa imesema kuwa itaanza kuondoa majeshi yake mwezi Machi.

https://p.dw.com/p/17Yfq
Rais Francois Hollande akishikana mkonona rais wa muda wa Mali Dioncounda Traore wakati wa ziara yaken nchini humo hivi karibuni.Ufaransa imesema itaondoa majeshi nchini Mali kuanzia mwezi Machi.
Rais Francois Hollande akishikana mkonona rais wa muda wa Mali Dioncounda Traore wakati wa ziara yaken nchini humo hivi karibuni.Ufaransa imesema itaondoa majeshi nchini Mali kuanzia mwezi Machi.Picha: Reuters

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian alisema operesheni ya nchi yake ilyiochukua siku 26 imeua mamia ya wapiganaji wakati majeshi yake ya angani na ardhini yakiwafukuza kutoka katika ngome zao kaskazini na kuelekea eneo la mbali lenye milima kaskazni mashariki, karibu na mpaka wa Algeria. Wizara ya ulinzi ilisema wapigaanji hao waliuawa katika mashambulizi ya ndege za Ufaransa dhidi ya magari ya kusafirisha wapiganaji wa vifaa, na katika mapambano ya moja kwa moja katika miji muhimu ya kati na kaskazini, ya Konna na Gao.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton akimtizama waziri wa mambo ya nje wa Mali Tieman Coulibaly (kushoto) walipohutubia kwa pamoja mkutano wa waandishi wa habari baada ya kikao cha kujadili msaada kwa nchi hiyo kilichofanyika mjini Brussels, Ubelgji. Wengine ni Kamishna na amani na usalama wa Umoja wa Afrika Ramtane Lamamra (wa pili kushoto) na naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala yakisiasa, Jeffrey Feltman (kulia).
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton akimtizama waziri wa mambo ya nje wa Mali Tieman Coulibaly (kushoto) walipohutubia kwa pamoja mkutano wa waandishi wa habari baada ya kikao cha kujadili msaada kwa nchi hiyo kilichofanyika mjini Brussels, Ubelgji. Wengine ni Kamishna na amani na usalama wa Umoja wa Afrika Ramtane Lamamra (wa pili kushoto) na naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala yakisiasa, Jeffrey Feltman (kulia).Picha: picture alliance/AP Photo

Kifo kilichotokea kwa Ufaransa hadi sasa ni cha rubani wa helikopta aliyeuawa wakati wa kuanza kwa operesheni ya kijeshi. Mali ilisema wanajeshi wake 11 wameuawa na 60 kujeruhiwa baada ya vita vya mji wa Konna mwezi uliyopita, lakini tangu wakati huo haijatoa idadi mpya ya vifo. Le Drian alisema jeshila Mali liliwachukua mateka baadhi ya wapiganaji ambao watashtakiwa katika mahakama nchini humo na kimataifa. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa,Laurent Fabius, alisema nchi hiyo itaanza kuondoa wanajeshi kuanzia mwezi Machi kama kila kitu kitakwenda vizuri.

Ni wakati wa suluhu ya kisiasa

Rais wa Ufaransa Francois Hollande, alisema baada ya kurejesha eneo la kaskazini kwa serikali, kinachotakiwa ni kufanya mazungumzo na waasi ili kuwa na amani ya kudumu."Natangaza kuwa kwa kuwa Mali imerejesha uhuru wake wa mipaka, sasa serikali ya nchi hiyo inayo nafasi ya suluhu ya kisiasa, nafasi ya kufanya mazungumzo na maridhiano, na kuleta utulivu katika nchi hiyo na kanda nzima ya Afrika Magharibi."

Karibu wanajeshi 4,000 wa Ufaransa wapo nchini Mali na mtawala huyo wa zamani yuko makini kukabidhi operesheni hiyo kwa vikosi vya Umoja wa Afrika, huku kukiwa na waswasi kuwa wapiganaji hao wanaweza kuanzisha uasi wa muda mrefu. Waasi wamekimbilia eneo la Adrar des Ifoghas massif, karibu na mji wa Kidal, eneo lenye milima yenye mapango ambako wanaaminika kuwashikilia mateka wafaransa saba. Moja ya makundi ya waasi-- Vuguvugu la Umoja na Jihadi katika Afrika Magharibi, MUJAO, lilisema limeshambulia vituo vya kijeshi mjini Gao, madai yaliyokanushwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika.

Rais Francois Hollande akishikana mkonona rais wa muda wa Mali Dioncounda Traore wakati wa ziara yaken nchini humo hivi karibuni.Ufaransa imesema itaondoa majeshi nchini Mali kuanzia mwezi Machi.
Wanajeshi wa Mali.Picha: Reuters

Wakati hayo yakijiri, mjini Brussels Ubelgji, mashirika ya kimataifa yakiwemo Umoja wa Mataifa na Umoja Afrika, yalikutana kujadili msaada kwa nchi hiyo, pamoja na uchaguzi wa kidemokrasia na kuhakisha usalama baada ya kuondolewa na waasi.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/afpe
Mhariri: Saum Yusuf