1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa kujadili uingiliaji kati Syria

3 Septemba 2013

Kwa mataifa matatu yenye kura ya veto katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa nia yao ni kuishambulia Syria. Lakini inaonekana pia kuwa hali inakwenda kinyume na matakwa yao.

https://p.dw.com/p/19aYG
French President Francois Hollande answers questions during a debate at the European Parliament in Strasbourg, February 5, 2013. REUTERS/Christian Hartmann (FRANCE - Tags: POLITICS)
Rais wa Ufaransa Francois HollandePicha: Reuters

Uingereza imejitoa baada ya wabunge kupinga hatua dhidi ya Syria. Marekani nayo, inataka pia kupata idhini kutoka kwa wabunge wake , hali ambayo matokeo yake hayajulikani. Ufaransa kwa muda wa siku kadha sasa inajaribu kuweka muungano wa kuishambulia serikali ya Bashar al-Assad, na majadiliano yamekuwa makali.

Bunge la Ufaransa linataka kujadili suala hilo na kutoa maamuzi kupitia vyama vyote. Kwa Ufaransa hata hivyo kuna wingi wa kutosha kufikia makubaliano, lakini wabunge wanajiuliza ni vipi itawezekana?

General view of the French parliament during the debate of the Armenian Genocide in Paris, Thursday, Dec. 22, 2011. Lawmakers are to vote on a measure that would make it a crime in France to deny that the mass killings of Armenians in 1915 amounted to a genocide, a measure that could put France on a collision course with Turkey, a strategic ally. Turkey wants the killings left to historians and has lashed out at France, warning that it will withdraw its ambassador if the measure becomes law.( AP Photo/Michel Euler)
Bunge la Ufaransa mjini ParisPicha: dapd

Mawazo yatofautiana

Si kawaida kwamba mawazo ya wengi yanakwenda kinyume na nia ya rais, amesema mwenyekiti wa chama cha upinzani cha UMP Jean-Francois Cope. Rais Hollande anawajibika kutoa ufafanuzi wa hali ilivyo kwa sasa pamoja na mipango yake.

Alain Juppe kiongozi mmojawapo mwenye ushawishi kutoka upinzani , ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya kigeni anapendelea kuingilia kijeshi nchini Syria. Pamoja na hayo anataka kwanza bunge lijadili na kutoa maamuzi. Itakuwa mara ya kwanza kwa Ufaransa kuingilia kati bila ya kupata idhini ya Umoja wa Mataifa.

French Foreign Minister Alain Juppe speaks to the media during a news conference with his Turkish counterpart Ahmet Davutoglu, unseen, in Ankara, Turkey, Friday, Nov. 18, 2011. Juppe on Friday called on the U.N. Security Council to act against Syrian President Bashar Assad's regime and said the time has come to strengthen sanctions against Syria over its brutal crackdown on civilians. Juppe said France has called on Assad to change but "the regime did not want to know, which is not acceptable." (Foto:Burhan Ozbilici/AP/dapd)
Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni Alain JuppePicha: dapd

Hii itakuwa ukiukaji wa sera zetu hadi sasa. Lakini nafikiri itatosha kwa bunge kuidhinisha, amesema Juppe.

Katiba haimlazimishi rais wa Ufaransa kupata idhini ya bunge kwenda vitani, anasema mbunge wa chama cha Kisoshalist Matthias Fekl alipozungumza na DW. Ama katiba pia haimlazimishi kuitisha kikao cha bunge kwa ajili ya suala kama hilo.

Hollande kufafanua hali ilivyo

Lakini rais Francois Hollande ameitisha kikao maalum cha bunge kesho Jumatano(04.09.2013). Anataka kulifahamisha bunge juu ya hali ilivyo nchini Syria pamoja na msimamo kwa upande wa kidiplomasia.

France's President Francois Hollande reacts as he delivers a speech during the annual Conference of Ambassadors at the Elysee Palace in Paris August 27, 2013. President Hollande said on Tuesday that France stood ready to punish the perpetrators of a chemical attack in Damascus last week and would increase its military support to the Syrian opposition. REUTERS/Kenzo Tribouillard/Pool (FRANCE - Tags: POLITICS)
Rais Francois HollandePicha: REUTERS

Haki ina upande mmoja tu. Pamoja na hayo kuna hali ya dharura, kuweza kujenga muungano na kupeleka majeshi kupambana nchi za nje, na kwamba sio uamuzi uliochukuliwa na nchi pekee, amesema mbunge wa bunge la Ujerumani anayezifahamu siasa za Ufaransa Andreas Schockenhoff. Nafahamu ulazima wa bunge la Ufaransa kukutana na kujadili suala hili, ameongeza mbunge huyo.

Inaonesha kuwa katika masuala kama haya wananchi pamoja na wabunge wao si lazima kuwa wana mawazo yanayofanana, ameeleza Schockenhoff katika mahojiano na DW. Hata katika mataifa ambayo katiba haijaeleza wazi juu ya mjadala wa bunge , kuna hali ya kupendelea mjadala wa wazi.

Mbunge wa Ufaransa Matthias Fekl ameongeza kuwa hakuna mtu anayetaka vita lakini kutokana na hili lililotokea Ufaransa inawajibu wa kuchukua.

"Wafaransa wana hisia sawa kama Wajerumani. Hatutaki vita, hatutaki uingiliaji kati kijeshi kwa gharama yoyote ile. Lakini hatutaki pia kuona wauaji wakiachwa bila kuadhibiwa".

Syria's president Bashar al-Assad gestures during an interview with French daily Le Figaro in Damascus in this handout distributed by Syria's national news agency SANA on September 2, 2013. REUTERS/SANA/Handout (SYRIA - Tags: CONFLICT CIVIL UNREST POLITICS ) ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WAS PROVIDED BY A THIRD PARTY. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS PICTURE IS DISTRIBUTED EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS
Rais Baschar al-AssadPicha: Reuters

Majeshi tiifu kwa rais Bashar al-Assad yamefanya shambulio la silaha za kemikali mwezi uliopita, ripoti ya kijasusi ya Ufaransa imesema, huku kiongozi huyo wa Syria akionya kuwa shambulio la kijeshi dhidi yake huenda likazusha vita vya eneo hilo lote.

Mwandishi : Heinze , Hendrik / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Hamidou Oummilkheir