1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yalenga kujiimarisha dhidi ya Uswisi

17 Juni 2016

Ufaransa wametinga hatua ya 16 za mwisho lakini kocha Didier Deschamps anafahamu kuwa watastahili kucheza vyema kama wanataka kupata ushindi katika dimba hilo linaloandaliwa nchini mwao

https://p.dw.com/p/1J8zH
Frankreich Fußball-EM Frankreich vs. Albanien in Marseille
Picha: Reuters/Y. Herman

Les Bleus wanakutana leo usiku na Uswisi katika mtanange wao wa mwisho wa Kundi A mjini Lille baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Romania na mwingine wa 2-0 dhidi ya Albania ili kutinga hatua ya mtoano.

Lakini kumaliza wa kwanza katika kundi ina maana kucheza dhidi ya timu iliyomaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi jingine, hivyo mpambano dhidi ya Uswisi bado ni muhimu wakati Ufaransa ina pointi sita nayo Uswisi nne. Kitu kingine muhimu kwa Ufaransa ni kuwa waache kupata ushindi mgumu na badala yake wajimwaye uwanjani. Kiungo N'Golo Kante anasema ni sharti waendelee kuimarika kama timu "Kitu muhimu ni kushinda, hicho ndicho tulifanikiwa kukifanya. Kufuzu haraka baada ya mechi mbili, baada ya hapo mchezo utaendelea kuimarika. Tutajaribu kuimarika katika mchuano unaofauata, lakini sijasikitika. Tunafahamu hatukucheza vyema kipindi cha kwanza dhidi ya Albania na tutajaribu kucheza nmchuano ujao kama tulivyofanya kipindi cha pili

Euro 2016 Rumänien vs Schweiz Embolo
Romania ni lazima wapate ushindiPicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Katika mechi zote mbili Ufaransa ilipata ushindi katika dakika za mwisho mwisho, kitu ambacho beki Samuel Umtiti anasema wanapaswa kukibadilisha katika mchuano unaofuata "nadhani sisi ni timu imara, nadhani hali yetu ya kiakili haiwezi kulaumiwa kwa sababu tutapambana hadi mwisho. Tumeona hili katika mechi za karibuni, hivyo ni vizuri maana sasa tunajua uwezo wetu katika kiwango hiki. Lakini nadhani tunaweza kujihakikishia ushindi wa mapema badala ya kusubiri hadi mwisho. Uswisi walisumbuliwa sana kwa kutoka sare ya 1-1 na Romania siku ya Jumatano lakini kocha Vladmir Petkovic tayari anaweka mikakati ya 16 za mwisho, maana wameweka guu moja katika hatua ya mchujo.

Albania wamepata sifa lakini hawajapata pointi kufikikia sasa kutokana na juhudi zao na hilo lazima libadilike wanaposhuka dimbani leo dhidi ya Romania mjini Lyon kama wangetaka kuepuka kufungishwa virago mapema

Kama watapa ushindi dhidi ya Romania basi Albania wanaweza kuwa na nafasi ya kuwa moja ya timu nne bora zitakazomaliza katika nafasi ya tatu kwenye Makundi yao ili kufuzu katika hatua ya 16 za mwisho.

Ufaransa ina pointi sita, Uswisi ina nne, na tayari hawakamatiki. Romania pia wanaweza kufuzu au waende nyumbani, kwa sababu matokeo ya sare yanaweza kuwaweka katika nafasi ya tatu na pointi mbili, na haitatosha kuwafikisha katika awamu ya mchujo. Lakini ushindi unaweza kuwapa pointi nne ambapo wanaweza kufuzu katika nafasi ya pili – kutokana na tofauti ya mabao au mabao yatakayofungwa ikiwa Ufaransa itailaza Romania katika mchuano mwingine.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef