1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yazilaumu nchi Ulaya

20 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CeEw

PARIS.Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Herve Morin amezilalamikia nchi nyingine wanachama wa Ulaya kwa kuchelewa kutoa askari kwa ajili ya kikosi cha umoja huo kulinda amani nchini Chad.

Kikosi hicho kilipangwa kupelekwa kwenye eneo lenye mzozo la Mashariki mwa Chad mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, lakini kimeshindwa kupelekwa kutokana na nchi hizo kuchelewa kutoa askari pamoja na vifaa kama vile helkopta.

Wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Dermot alielezea uhakika wake ya kwamba kikosi hicho cha Umoja wa Ulaya kitapelekwa nchini Chad katikati ya mwezi ujayo.

Lakini maafisa wa Umoja huo hapo jana walisema kuwa bado kuna upungufu wa vifaa baada ya kuwasiliana upya na nchi zinazochangia kikosi hicho na kwamba hakuna tarehe iliyopangwa kwa kikosi hicho kwenda Chad.