1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufumbuzi wa Katiba ya Ulaya ?

15 Mei 2007

Katiba ya Ulaya yabainika imezikwa na mahala pake ni mkataba wa kimsingi wa Ulaya.Hilo laweza kuwa suluhisho la kutoidhinishwa katiba hiyo na nchi kama Ufaransa na holland.

https://p.dw.com/p/CHEL

Je, utapatikana sasa ufumbuzi kuidhinishwa katiba ya Umoja wa Ulaya ?

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani, mwanzoni mwa kipindi chake cha miezi 6 kama rais wa Umoja wa Ulaya , aliahidi kusaka njia ya kuikwamua katiba ya ulaya .Kwani, katiba hiyo tangu kura ya maoni ya wananchi huko Ufaransa na Holland kuikataa imekwama.Jana basi, walikutana wajumbe maalumu wanaohusika na mada hii kutoka nchi 27 zanachama ili kuzingatia jinsi gani kuikwamua.

Shinikizo la kuidhinisha haraka katiba hiyo linazidi.Kwani, muda wa Ujerumani wa kuendelea kuwa mwenyekiti wa UU umesalia wiki 5 tu ili Kanzela Merkel atimize shabaha yake kuu alioiweka alipochukua wsadhifa huu mapema mwaka huu.

Kuna mabadiliko tayari yaliokwishafanyika.Kwa mfano neon katiba halipo tena.Waingereza hawakulitaka kabisa,kwavile wao kwao hawana katiba.Na pia nchi nyengine zanachama na hasa zile kutoka Ulaya ya mashariki,wanapinga chochote kile kitoacho sura ya kuwa na dola kuu la Ulaya litakalozipokonya mamlaka yao.Kwa mfano hatiridhiani kuwa wimbo wa taifa wa UU ,bendera moja au vitambulisho vyengine.

Jambo moja wanakubaliana nalo wote kuwa mkataba mpya wa kuongoza UU ambao utaitwa sasa kwa jina hilo,utaingiza sio mambo mengi kama ilivyopangwa katika katiba.

Hivyo ni kusema mikasi imepitishwa katika katiba ya zamani:Uingereza kwa mfano ingependelea mkataba wa kimsingi.Na hasa rais mpya wa Ufaransa Nicolas Zarkozy angependelea mkataba mdogo tu ili aweze kuupitisha bungeni kama mageuzi madogo katika umbo la UU.Ni hapo tu yuko tayari kuafikiana.

Wanachama wote pia wanaafikiana kuwa taasisi zinazoendesha UU zinahitaji kufanyiwa mageuzi.Swali mageuzi hayo yawe makubwa namna gain na yafike wapi ?

Kanzela Angela Merkel asema:

“Kuna masilahi tofauti kuzingatiwa.Na hakuna shaka juu ya hilo.”

Poland kwa mfano ingependelea kuona suluhisho lililofikiwa kwa taabu miaka 2 nyuma juu ya nguvu za upigajikura kwa kila m wanachama kuzingatiwa upya.Kanzela Merkel hapo itampasa kutia munda ,kwani ikifanyika jaribio kama hilo jingo zima litaporomoka.

Sio tu hakutakua na mkataba mdogo wa UU,bali hakutakua na chochote tena cha kuafikiana.Maombi mengine kama vile, kuwa na msimamo mmoja katika ulinzi wa mazingira na hali ya hewa na mshikamano katika nishati ni rahisi kuyaitikia.

Ombi la Holland kuruhusu mabunge ya nchi zanachama kutia munda kwa kura ya turufu-veto, sheria za UU halitawezekana.Mabingwa wa Ulaya na wa maswali ya sheria wa Kanzela Angela Merkel, watakuwa na kazi ngumu wiki zinazokuja kufumbua tofauti zote zitazoibuka ili kuridhisha kila mwanachama.

Kwa mfano, wapi unaishia mpaka wa wanachama wa UU kama inavyodai Holland wakati Uingereza ingependelea kuona Umoja huo unazidi kupanuka.

Mafanikio ya juhudi zao, yanahatarishwa na dola 2 zisizo na shauku kuu na Umoja wa Ulaya: Tony Blair,waziri mkuu wa Uingereza anaen’gatuka, angependa kuona Uingereza inaregeza kamba,lakini hajui iwapo mrithi wake madarakani angeridhia hayo.Na serikali ya Poland mjini Warsaw, inafahamika kwa jumla,haibashiriki itachukua msimamo gani .