1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda kuchunguza zaidi wizi wa misaada ya wakimbizi

16 Februari 2018

Uganda imesema inapanua uchunguzi wa viongozi wa serikali ambao wanadaiwa kuiba misaada ya wakimbizi na kuhusisha wafanyakazi wa umoja wa mataifa, huku wasiwasi ukiongezeka juu ya uwezekano wa wafadhili kukata misaada.

https://p.dw.com/p/2spUY
Uganda Bürgerkrieg und Hunger im Südsudan treiben Menschen zur Flucht
Picha: Getty Images/D. Kitwood

Madai ambayo viongozi wanaweza kuwa  wameingizwa  katika tuhuma hizo,   ni aina nyingine ya udanganyifu iliyowakasirisha wafadhili na kuiaibisha nchi hiyo inayopokea  idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Sudan ya kusini.

Waziri wa misaada,  maafa  na wakimbizi Hilary Onek amewaambia waandishi wa habari kwamba wanachunguza watu wote zikiwamo jumuiya za kimataifa kama kulikuwa na ushirikiano na wafanyakazi wao.

Waziri huyo alipoulizwa kama uchunguzi huo utahusisha shirika la umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani WFP pamoja na shirika la kuwahudumia wakimbizi UNHCR akasema kuwa watu wote hao watapitiwa na uchunguzi.

Uganda Solidarity Summit on refugees
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akisiliza jambo kutoka kwa wakimbizi akiwa na waziri mkuu wa Uganda Ruhakana Rugunda, Juni 22, 2017.Picha: Getty Images/AFP/M. O´Hagan

Msemaji wa UNHCR aliepo Geniva Uswis Babar Baloch amesema wawakilishi wa mashirika ya umoja wa mataifa wanatakiwa kutoa ushirikiano katika uchunguzi utakaofanyika nchini Uganda kuhusu kashfa hiyo.

Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR  limesema wiki iliyopita kuwa linatazamia kuona Uganda inapambana na rushwa na udanganyifu.

Idadi ya wakimbizi waliopo

Uganda inasema mpaka sasa inawahifadhi wakimbizi wapatao milioni 1.4, huku zaidi ya milioni wakitokea Sudani kusini ambapo mwaka wa nne wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamewakimbiza nusu ya raia waliopo nchini humo.

Raia wengine wa Sudan Kusini wanakimbilia nchi jirani za Burundi na Jamhuri ya kidemekrasia ya Congo DRC.

Uganda iliheshimiwa sana kwa kufungua mipaka yake, kuwapa wakimbizi  shamba la kilimo  na kuruhusu uhuru wa bure na haki za ajira.

Lakini kupanda kwa idadi ya wakimbizi kumezidi fedha za msaada zilizopo na WFP ililazimika kupunguza mgao wa chakula mwaka jana.

Uganda Flüchtlinge aus dem Südsudan
Wakimbizi wa Sudan Kusini wakiwasili katika kambi kaskazini mwa Uganda.Picha: UNHCR/I. Kasamani

 Chanzo cha kidiplomasia cha magharibi mwa Kampala kiliwaambia waandishi wa habari wa shirika la Reuters kuwa UNHCR imewataarifu wafadhili huko  Geneva january 19 juu ya madai ya usimamizi mbovu wa misaada ya wakimbizi na baadae umoja wa mataifa ukaitaarifu serikali ya Uganda.

Viongozi watano wa ofisi ya waziri mkuu tayari wamesimamishwa kazi.

 Balozi wa Marekani nchini Uganda Debora Malac amewaambia maafisa wa Uganda mwanzoni mwa mwezi Feb. kuwa wanatakiwa kulipa kiasi cha pesa kilichoibbiwa nakuwafungulia mashikata wanaohusika.

Mwandishi: Veronica Natalis/Reuters

Mhariri: Iddi Ssessanga