1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takribani waasi 200 walikuwa wamehifadhiwa nchini Uganda

17 Januari 2017

Zipo taarifa kuwa kiasi ya waasi 200 wa kundi la M23 walokuwa wamehifadhiwa nchini Uganda wamevuka tena na kuingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

https://p.dw.com/p/2VvQk
Kongo FARDC Soldaten
Picha: Getty Images/AFP/J. D. Kannah

Jeshi la Uganda limekanusha taarifa kwamba takriban waasi 200 wa kundi la M23 waliopewa hifadhi nchini humo wamevuka mpaka na kuingia tena katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Uganda meja Henry Obbo amesema kwamba wapiganaji hao bado wako katika kambi ya kijeshi ya Bihanga iliyoko kilomita 320 magharibi mwa mji mkuu wa Kampala. Msemaji wa serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Lambert Mende aliwaambia waandishi wa shirika la habari la AFP kwamba waasi hao wa Kitutsi waliingia nchini humo na kukiteka kijiji kimoja katika jimbo la Kaskazini la Kivu. Waziri wa mambo ya nje wa Uganda Henry Okello Oryem amesema Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo haipaswi kutafuta visingizio kwa kuwahusisha waasi hao wa M23.