1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yasonga mbele AFCON

1 Julai 2019

Kombe la Mataifa barani Afrika linaendelea Misri Jumapili kulichezwa mechi za mwisho za kundi A na B na kwenye kundi B Madagascar wanaoshiriki kinyang'anyiro hiki kwa mara ya kwanza waliwalaza Nigeria 2-0.

https://p.dw.com/p/3LPxy
Afrika-Cup 2019 | Uganda vs. Ägypten
Picha: picture-alliance/dpa/O. Zoheiry

 Kwa ushindi huo Madagascar walishika uongozi wa kundi lao huku Nigeria wakiwa wa pili.

Kwenye kundi A Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilipata ushindi mkubwa wa magoli mane kwa bila dhidi ya Zimbabwe. Ushindi huu unawapa matumaini Congo licha ya kulazwa katika mechi zao mbili zilizopita kwamba wanaweza kufuzu kwenye hatua inayofuata kama mojawapo ya timu nne bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu.

Cedric Bakambu ambaye alifunga magoli mawili ndiye aliyekuwa mchezaji bora na alikuwa na haya ya kusema baada ya mechi.

"Kwetu sisi lengo lilikuwa kufunga magoli mengi usiku wa leo. Magoli mawili kwa bila ulikuwa uongozi mzuri ila si wa kutosha. Tulipokuwa tunaongoza mbili bila kwenye muda wa mapumziko, tulizungumza na tukaelezana kwamba tunaweza kufunga magoli mengi zaidi. Tulifanya hivyo na nafurahia sana," alisema Bakambu.

Mechi nyengine ya kundi hilo ilishuhudia Misri kupata ushindi wa tatu mfululizo kwa kuwacharaza The Cranes wa Uganda mabao mawili kwa bila Mohammed Salah na El Mohamady wakiwafungia The Pharaohs magoli yao. Uganda lakini wamefuzu licha ya kupoteza mechi hiyo.