1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki na Ureno zimezongwa na madeni

28 Aprili 2010

Uchumi dhaifu nchini Ugiriki na Ureno umeathiri thamani ya hisa katika masoko ya fedha barani Ulaya na Marekani.

https://p.dw.com/p/N8JV
Police clash with protesters in Athens on Wednesday Feb. 24, 2010. Police fired tear gas and clashed with demonstrators in central Athens on Wednesday as violence broke out after a large protest march against government austerity measures intended to fix the country's debt crisis. (AP Photo/Thanassia Stavrakis)
Waandamanaji wanaopinga mpango wa serikali ya Ugiriki kupunguza matumizi yake.Picha: AP

Kwa mujibu wa "Standard and Poor" taasisi inayotathmini uwezo wa nchi kulipa madeni yake, Ugiriki na Ureno zimetiwa katika kundi lenye hisa zisizo na thamani. Kwa hivyo sasa ni vigumu zaidi kwa serikali ya Ugiriki iliyobanwa kwa madeni, kupata mikopo katika masoko ya fedha. Riba inayodaiwa kwa hati zake za miaka kumi, imefikia takriban asilimia 10.

Sasa inazidi kudhihirika kuwa Ugiriki itahitaji kupewa msaada wa fedha uliopangwa na Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, ili kuinusuru nchi hiyo kwenda muflis.Jumatano ya hii leo,wajumbe wa serikali ya Ujerumani, IMF na Benki Kuu ya Ulaya, wanakutana mjini Berlin kushauriana njia ya kuisaidia Ugiriki iliyobanwa kwa madeni.

Kwa upande mwingine Wagiriki hiyo jana walimiminika katikati ya mji mkuu Athens kupinga hatua kali zilizopangwa kuchukuliwa na serikali yao katika jitahada za kubana matumizi.Vile vile migomo imepangwa kufanywa tarehe mosi mwezi Mei katika mjini Athens na mgomo mkuu utakuwa tarehe 5 Mei.

Mwandishi:Martin,Prema/DPA