1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhaba wa majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR)

16 Desemba 2008

Majaji saba kati ya 18 wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), watakuwa wamejiuzulu ifikapo Desemba 31, mwaka huu na kuiacha mahakama hiyo katika ukakasi mkubwa wa utekelezaji wa kazi zake.

https://p.dw.com/p/GHMk

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo mahakama hiyo inatakiwa kuanza kusikiliza kesi mpya 10 kuanzia Januari mwakani, huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiitaka mahakama hiyo kuhitimisha kazi zake ifikapo Desemba, mwakani.

Mwandishi wetu kutoka Arusha, Nicodemus Ikonko ana taarifa zaidi.