1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhariri wa DW juu ya Cote d'Ivoire

Saumu Ramadhani Yusuf17 Desemba 2010

Je nchi hiyo itarudi tena katika vita vya wenyewe kwa wenyewe?

https://p.dw.com/p/Qeo4
Picha: AP

Tangu kumalizika uchaguzi wa rais mwishoni mwa mwezi wa Novemba huko Cote d´Ivoire nchi hiyo imeingia katika mgogoro. Hapo jana kiasi ya watu 20 waliuwawa kufuatia mapigano yaliyoibuka. Nchi hiyo iko katika hali inayokaribia kuitumbukiza kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, na anayenyooshewa kidole cha lawama kwa kubeba dhamana ya  hali hiyo nzima ni rais anayetakiwa kuondoka madarakani Laurent Gbagbo.

Niko hapa na nitaendelea kubakia hapa. Kutokana na matamshi hayo ya Laurent Gbagbo ni wazi kwamba alikuwa ameshapanga toka mwanzo lengo lake kabla ya uchaguzi. Rais huyo wa zamani kwa hivyo hakuwa na mpango mwingine mbadala. Na juu ya hilo anaendeleza shinikizo katika barabara za nchi hiyo akiwatoa majiani wafuasi wake vijana  kumpinga mpinzani wake Allasane Quattarra.

Kinyang'anyiro hiki cha kugombea madaraka ambacho sasa kimeiweka pabaya Cote d´Ivoire kimesababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa. Hali hiyo ilikuwa imeshajitokeza hata kabla ya uchaguzi. Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalikuwa yameshamalizika rasmi.

 Lakini sasa katika hali kama hii kundi la wachache la wanasiasa linajikuta katika hali kama iliyopita kwamba wanageuka kuwa wachocheaji na washiriki katika vita, ambao kwa hali yoyote wanaonekana pamoja na vyama vyao vya kisiasa kuwa watu wasikuwa na mwelekeo na zaidi kwao wameshajiandaa kwa hali yote kuingia vitani.

Mfumo wa kuwagawanya watu na kutawala ndio uliokuwa unatumika nchini humo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Kufuatia hilo pamezuka makundi ya kisiasa yanayofaidika na hali hiyo. Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yameyanufaisha makundi mbali mbali na madini ya nchi hiyo. Waasi walioko Kaskazini ndio walioko katika nafasi ya kunufaika na utajiri wa almasi na dhahabu kwa kuendesha biashara haramu ya madini hayo. Katika eneo la Kusini waasi wa huko nao wananufaika kutokana na zao la Kakao pamoja na bidhaa nyinginezo za  kilimo.

Wanaochochea mapigano ni wengi nchini Cote d´Ivoire. Wanasiasa wa kweli wenye nia ya kuiweka nchi hiyo katika mfumo wa Demokrasia na kuyagawa madini kwa kuzingatia haki ni wachache mno. Kwa hivyo nchini Cote d´Ivoire hakuna mapatano na hakuna kugawana madaraka. Hakuna vyombo vya habari visivyoegemea upande wowote na wala mahakama huru. Na kutokana na hilo ndio sababu kuna matatizo ya kijamii  na hakuna anayeweza kweli kuikoa nchi hiyo isitumbukie tena katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Mwandishi: Schaeffer Ute/Saumu Yusuf/ZPR

Mhariri Josephat Charo